Uzembe
na kutojali kwa baadhi ya wananchi wanaotumia vifaa vya moto imetajwa kuwa ndio
sasabu inayosababisha kuendelea kutokea
kwa mlipuko wa moto katika sehemu mbalimbali hapa nchini
.
Akiongea
na Karagwe Forum mkuu wa kikosi cha zima moto wilaya ya Karagwe Koplo Peter
Mbale amesema kuwa vitendo vya kulipuka moto ambavyo vinazidi kujitokeza katika
sehemu nyingi vinatokana na watumiaji kuwa wazembe na wengine kutojali kabisa
juu ya madhara yanayotokana na moto.
Mbale
amezungumzia mlipuko wa moto ambao ulitokea mei16 mwaka huu katika nyumba ya
Peragia Philimoni mkazi wa kata ya Kayanga na kuunguza chumba na sebure moja na
vitu vilivyokuwemo ulisababishwa na uzembe ambapo mhusika aliacha pasi ya mkaa
chini ya kiti ndipo moto ulishika kiti hicho na kuanza kuunguza vitu vingine.
Ameongeza
kuwa ni vema watu wachukue tahadhari na kuzingatia elimu na ushauri wanaopata
kutoka kwa viongozi wa zima moto kwani kuna madhara mengi ynatokea pale
kunapokuwepo na mlipuko wa moto sehemu husika.
Mbale
amewataka wananchi wa wilaya ya Karagwe kutambua kuwa sio kila moto unaotokea
unazimwa na gari zima moto kuna vifaa vingine vinatumika kuzima moto hasa ule
ambao unakuwa sio mkubwa huku akieleza kuwa licha ya kuwa tayari gari la zima
moto lipo lakini halijakamilika kwani bado halina tenki ya maji na utaratibu wa
kukamilisha unaendelea.
Post a Comment