Wakulima
wa zao la mpunga kata ya Ipinda katika kijiji cha kafundo wilayani Kyela mkoa wa Mbeya wameishauri
jamii kuwapatia kipaumbele wanawake wanaojihusisha na kilimo cha mpunga ili
kuwapa nafasi ya kutoa maamuzi katika kuendeleza gurudumu la maendeleo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wamesema wanawake wanaojihusisha na kilimo katika eneo la
kafundo hawajapewa nafasi ya kumiliki mashamba binafsi jambo ambalo limekuwa
moja ya sababu ya kumfanya mwanamke azidi kuwa nyuma katika harakati za
maendeleo.
Wameongeza
kuwa sababu kubwa inayochangia kumrudisha nyuma mwanamke katika sekta ya kilimo
ni pamoja na kukosa elimu juu ya umuhimu wa kumiliki mashamba mbali na
kumtegemea mwanaume.
Kwa
upande wake afisa kilimo kata ya Ipinda katika kijiji cha kafundo Theresia
Simbeye amesema katika kijiji cha kafundo wanawake baadhi hawajapata nafasi ya
kumiliki aridhi kwa ajili ya kilimo kutokana na ukinza kwamba mwanamke hawezi
kuendesha shughuri za kilimo na kumilik aridhi
Post a Comment