Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Kyela Daktari Hanta Mwakifuna amewataka vijana
mbalimbal wilayani humo kuwa watulivu juu ya pesa ya ahadi ya Raisi ya shilling
million 50 kwa kila kijiji itakayo wahusu vIjana wa jinsia zote ili
kuwasidia katika suala la maendelo.
Akizungumza na
mwandishi wa habari ofini kwake amesema pesa hizo zitawawahusu vijana
wote bila kujali jinsia katika ugawaji huo na kuzingatia vigezo vya vijana hao
katika upataji wa pesa hizo.
Ameongeza kuwa wao
kama serikali bado hawajapata muongozo wa kuwezesha kugawa fedha hizo katika
makundi ya vijana hao na kusisitiza kuwa pesa hizo bado hizijaingizwa tamissemi
kwa ajili ya ugawaji wa pesa hizo.
.
Itakumbukwa kuwa pesa
hizo ziliahidiwa na Rais John Pombe
Magufuli katika kampeni zake kwa ajili ya kutekeleza ilani ya chama cha
mapinduzi.
Post a Comment