Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WATU WAWILI MKOANI KAGERA WAPOTEZA MAISHA KWA MATUKIO TOFAUTI WENGINE NI WIVU
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
WATU wawili wamekufa Mkoani KAGERA kwa matukio mawili tofauti likiwemo la aliyeuawa na mpenzi wake kwa kichomwa na kisu kifuani.   Kam...

WATU wawili wamekufa Mkoani KAGERA kwa matukio mawili tofauti likiwemo la aliyeuawa na mpenzi wake kwa kichomwa na kisu kifuani.
 
Kamanda wa polisi mkoani KAGERA AGUSTINE OLLOMI amesema  tukio la kwanza limetokea  katika kijiji cha Lukole kata ya Ihanda Wilayani Karagwe ambapo kijana mmoja aitwaye Eliudi Jonas (27) anashikiliwa na jeshi la polisi bada ya kumuua mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Georgina Frances (56) anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
 
Amefafanua kuwa  tukio hilolimetokea Mei 16 mwaka huu saa nane usiku ambapo wapenzi hao walikuwa na mfarakano ndipo Jonasi aliinuka kitandani na kuchukua kisu na kumchoma Georgina kifuania hari iliyopelekea kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha kabla ya kifikishwa hopsitali.
 
Kwa mujibu wa kamanda OLLOMI  baada ya mtuhumiwa huyo kufanya tukio hili alitoroka ambapo Mei 17 polisi wakiendelea na msako walimnasa na upelelezi bado unaendelea atafikishwa mahakamania muda wowote.
 
Katika hatua nyingine  Mei 17 saa tano asubuhi  katika kijiji cha Butembo kata ya Buleza wilaya ya Muleba ambapo Mtu mmoja ambaye hajajulikana jina umri kati ya (25-30)aliuawa na wananchi wasiojulika ambao walijichukulia sheria mkononi baada ya mtu huyo kuvamia na kuvunja nyumba  saba kisha kuiba vitu mbalimbali wakati wenye nyumba hao wakiwa katika kazi za mashambani.
 
Akizungumza naWaandishi wa habari  kamanda wa jeshi la polisi AGUSTINE OLLOMI amesema kuwa wananchi hao wamemushambulia kwa mawe marehemu huyo ndipo raia mwema alitoa taarifa polisi Muleba ambapo polisi kabla hawajafika wananchi walikimbia,   polisi wakafanikiwa kumchukua na kumkimbiza katika hospitali ya Wilaya hiyo lakini hari yake iliendelea kuwa mbaya na kufa baada ya muda mfupi.
 
Amebainisha  kuwa jeshi hilo linaendelea  kufanya uchunguzi ili kuwabaini wahusika  wachukuliwe hatu kwa mujibu wa sheria.
 
Wakati huo huo kamanda OLLOMI amesema  kuwa jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wasiojulikana waliochoma moto nyumba ya  Philemoni Mulokozi (54) ambapo vitu vyote vilivyokuwemo viliteketea kabisa pia  kusababisha hasara ya shilingi milioni 50.
 
Amesema kuwa  tukio hilo limetokea  Mei 16 mwaka huu katika eneo la Bomani kata ya kayanga Wilayani Karagwe

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top