MAELEZO YA KINA KUHUSU UFUNDISHAJI WA
DIPLOMA YA SAYANSI, HESABU NA TEHAMA
1. Utangulizi
Kuanzia Novemba 2014, Chuo Kikuu cha
Dodoma kilianza kupokea wanafunzi wa kusomea stashahada maalum ya diploma ya
Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama (DE-SMICT). Lengo kubwa la programu hii
maalum ni kutimiza azma ya serikali kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la
walimu wa sayansi katika shule za sekondari nchini. Serikali iliamua kuwaleta
wanafunzi hawa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) badala ya kupeleka kwenye vyuo vya
ualimu ikiamini kwamba UDOM kuna miundombinu ya kutosha hasa majengo na
rasilimaliwatu ya kutosha kuweza kuhifadhi wanafunzi hao. Menejimenti na
jumuiya nzima ya UDOM iliona ni heshima kupewa jukumu hili na kulipokea kwa
mikono miwili. Kukubaliwa na kupokelewa jukumu hili UDOM ililazimika kujipanga
upya kimkakati, kimfumo pamoja na kufanya mabadiliko kadha wa kadha katika
utendaji wake wa kila siku ili kuweza kuhimili jukumu hili kubwa la kitaifa.
Mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ilikuwa kuunda Kikosi Kazi (Steering
Committee- SC) cha kushauri namna ya kukabili jukumu hili.
1.1 Kuundwa Kamati Maalum ya Uratibu
(Steering Committee-SC)
Kuundwa kamati ya kuratibu
ufundishaji wa wanafunzi hawa (SC) ulionekana kuwa ni muhimu sana kutokana na
ukweli kwamba ni lazima kutafuta utaratibu tofauti wa utoaji taaluma kwa
vijana. Kamati hiyo iliundwa kwa kuwashirikisha Koleji, Skuli na Idara
zinazohusika na masomo ya sayansi, ualimu na TEHAMA.
Kwa msingi huu, Koleji za Elimu,
Sayansi asilia na Kumpyuta ndizo zilizohusika katika kuunda kamati hiyo. SC
iliyoundwa ilipewa jukumu la kuratibu namna bora ya kushughulikia masuala ya
taaluma, malazi, nk. na kupeleka mapendekezo ngazi za juu kwa maana ya
Menejimenti ya UDOM na vyombo vya maamuzi ya kitaaluma kama Udhibiti wa Ubora
(Quality Assurance) na Seneti ya UDOM (Senate).
Kabla ya kuanza kufundisha, SC
ilipendekeza mikakati, mifumo na mabadiliko yaliyokuwa ya msingi ili kukabili
swala hili. Changamoto kubwa, ilibainika ni, ufundishaji wa hawa vijana.
Masuala mengine yahusuyo malazi na malezi kwa ujumla wake yaliandaliwa ingawa
hayakuwa na changamoto kubwa kama suala la
UFUNDISHAJI. Suala la ufundishaji
lilihitaji jicho la pekee kwani vijana hawa waliopokelewa ndiyo kwanza
wamemaliza kidato cha nne, hivyo bado ni wadogo kwa kiasi fulani na pia
hawakupaswa kufundishwa kama wenzao wanaosomea masomo ya shahada na kuendelea.
Ifuatayo ni mikakati ya ufundishaji iliyoshauriwa na SC-UDOM ili kuweka
mazingira mazuri ya vijana hawa kusoma kwa ufanisi.
1.2 Ugawaji wa Mikondo (Streams)
Kama ilivyobainishwa hapo awali
kwamba ni lazima kutafuta utaratibu tofauti, kamati ya uratibu ilijadili kwa
kirefu na kwa kina namna ya kugawa wanafunzi katika mikondo inayoweza
kufundishika katika misingi na maadili ya utoaji taaluma na zaidi sana
kutofautisha utoaji wa taaluma kwa wanafunzi wanaosoma programu za diploma na
wale wanaosoma shahada. Sababu ya pili ni kwamba, masomo ya sayansi yanahitaji
uzito wa pekee tofauti na masomo ya sanaa yasiyohusisha vitendo katika maabara.
Baada ya mjadala mrefu, ilikubalika kugawanywa mikondo (streams) ya ufundishaji
kwa utaratibu ufuatao;
a. Masomo yote ya UALIMU yawe na
wanafunzi 120 katika mkondo mmoja.
b. Masomo yote ya SAYANSI ASILIA yawe
na wanafunzi 80 kwa mkondo mmoja.
c. Masomo yote ya TEHAMA yawe na
wanafunzi 60 kwa mkondo mmoja
2 Kwa mtiririko huo hapo juu, ina
maana kwamba kwa kila somo, itabidi wanafunzi wagawanywe katika mikondo kwa
idadi iliyokubalika na si kuwarundika wote sehemu moja. Utaratibu huu ndio
ulioonekana kutenda haki katika ufundishaji wa vijana hawa kwa kufuata misingi
na maadili ya utoaji elimu. Kamati hii ilianza kazi vizuri. Vijana takriban
2000 walipokelewa, wakafundishwa na (semester) huhula wa kwanza ukamalizika
vizuri bila migogoro mikubwa.
Pamoja na kasoro ndogo ndogo
zilizojitokeza katika semester/muhula wa kwanza (2014/15)
,
ufundishaji ulifanyika kwa ufanisi. Matatizo yalianza kujitokeza pale waalimu
walipotakiwa kulipwa kwa kufanya kazi ya ziada katika ufundishaji wa hawa
vijana. Kulingana na mapendekezo ya SC ambayo yalikuwa yamekubalika, kila
mwalimu aliyefundisha masomo ya DE-SMICT kama somo la ziadi alitakiwa kulipwa
Shilingi Milioni Moja (endapo tu somo hilo litakuwa ni ziada katika idadi ya
masomo anayoruhusiwa kufundisha). Mvutano wa kuwalipa waalimu hawa ulipelekea
wanafunzi kuchelewa kuanza masomo yao ya muhula wa pili kwa wiki mbili. Makamu
Mkuu wa Chuo (VC) alipoligundua hili aliamuru malipo yafanyike na baada ya
malipo wanafunzi walirejea madarasana na kazi ikaendelea. Mgogoro huu
ulipelekea aliyekuwa mwenyekiti wa SC ambaye ni Mkuu wa Koleji ya Elimu
kuondolewa katika wadhifa huu. Hatimaye Dean wa Skuli ya Elimu ya Ualimu
aliteuli[truncated by WhatsApp]
[5/30,
17:42] br kingu: Kutokana na ufanisi uliopatikana katika mwaka wa masomo
2014/15, Serikali na UDOM waliamua kuleta tena wanafunzi wengine kwa muhula wa
2015/16. Idadi ya hawa wanafunzi ni takriban 6000. Kulingana na idadi hii kuwa
kubwa mno, upatikanaji wa waalimu wa sayansi wanaoweza kuenea/kutosha mikondo
yote iliyogawanywa ulishindikana.
Hali
ya wingi mkubwa wa wanafunzi na upungufu mkubwa wa waalimu ililazimu kubuniwa
mbinu za ziada ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaingia madarasani. Kwa
maneno marahisi kabisa, kundi hili la pili lililodahiliwa na
3
kusajiliwa ambalo lilikuwa na wanafunzi takriban 6000, lilifanya UDOM
KUELEMEWA
na MZIGO. Koleji na Skuli zinazohusika kuwafundisha vijana hawa zilibeba MZIGO
uliowazidi kwa kilo/tani nyingi kuliko ilivyopaswa kubeba. Jedwali Namba 1 ni
ushahidi wa mzigo unaobebwa na idara mbalimbali;
Kwa
ushahidi uliotolewa katika jedwali Namba 1, yeyote hahitaji kutafuta elimu ya
ziada kugundua kwamba idara husika zimeelemewa na mizigo ya ufundishaji. Kwa
taarifa
tu, mgawanyo wa masomo ya ufundishaji ulioelezwa kwenye jedwali 1 hauhusishi
masomo ya Shahada, Diploma za kawaida, Astashahada, cheti na shahada za juu.
Hii inadhihirisha wazi kwamba, mzigo kwa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi
tayari umeshawazidi na bado wanahitajika kufundisha masomo mengine ya kawaida.
Kwa vyovyote vile, jitihada zozote za kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo
zililazimu kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya Menejimenti ya Koleji husika
na Utawala Mkuu wa Chuo yaani Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (DVC-ARC) na
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala (DVC_PFA). THTU na UDOMASA
ilishauri toka mwanzo umuhimu wa ushirikiano wa wadau mbalimbali ndani ya chuo
katika kulishughulikia suala la ufundishaji wanafunzi hawa. THTU ilitoa tamko
Januari 2015 kuelezea namna isivyoridhishwa na mtindo wa kushughulikia matatizo
yanayojitokeza. Tunaweka nukuu mbili tu kati ya mengi ya tamko hilo ambalo
lililalamikiwa sana na kufikia hatua ya kutaka kuwajibisha viongozi wa THTU.
Hali iliyoelezwa mwaka jana 2015 imejirudia tena mwaka huu 2016 na kuibua
mgogoro;
a.
Pia kwa nyakati mbalimbali chama cha wafanyakazi (THTU-UDOM) na jumuiya ya
wanataaluma (UDOMASA) mara kadhaa walishauri menejimenti ya chuo kushirikisha
wafanyakazi wa kada mbalimbali katika hatua zote za maandalizi ya programu hii
ili kuleta ufanisi katika kuwaandaa walimu hawa wa masomo ya sayansi.
b.
Tunaishauri menejimenti ya chuo na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi
kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa wanafunzi wa diploma ya
sayansi kwa kuleta vifaa vya maabara, vifaa vya kufundishia na kujifunzia,
usafiri ndani ya chuo, na kuwa na uratibu na usimamizi ulio wazi katika kila
idara na kada inayohusika moja kwa moja kuwahudumia wanafunzi hawa. Hii
itasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoibuliwa na wafanyakazi na
wanafunzi katika utoaji wa huduma.
2.
Kutumia Wafanyakazi wasio wanataaluma
Kutokana
na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi, kamati ya uratibu
ilipendekeza kwenye menejimenti ya UDOM kwamba wafanyakazi ambao si wanataaluma
lakini walisoma shahada ya masomo ya sayansi wapewe masomo ya kufundisha kwa
makubaliano ya kulipwa baada ya kazi. Wazo hili lilikubalika na kutekelezwa kwa
nia ya kutumia rasilimali watu iliyopo ndani ya UDOM badala ya kuwaleta watu
wengine kutoka nje ya UDOM. Hata hivyo, waswahili husema,
5
shukurani ya punda ni mateke. Methali hii imejidhihirisha katika hili baada ya
watu hawa walioombwa na Menejimenti ya UDOM kusaidia kupunguza upungufu wa
walimu wa sayansi kuishia kupewa barua za ONYO ya kwamba walijipa majukumu
yasiyowahusu.
3.
Jitihaada za uongozi wa Koleji ya Sayansi Kavu na Hisabati (CNMS)
Ili
kuhakikisha kuwa wanafunzi hawarudi nyumbani wala kwenda barabararani, uongozi
wa CNMS ulijitahidi kuushirikisha uongozi wa chuo na kuomba msaada kila
palipoonekana kuhitajika msaada huo. Baadhi ya maswala muhimu yaliyotakiwa
kushuhulikiwa ni kuwaongezea uwezo wa kupata waalimu wa ziada, kupata sehemu za
kufundishia na kupata vifaa vya maabara. Hata tunapoandika hivi sasa, DVC-PFA,
pamoja na kupokea nyaraka mbali mbali zinazomwomba aagize vifaa na madawa ya
maabara (laboratory equipments and reagents) hajanunua hata kitu kimoja. Wanafunzi
wamefundishwa bila kupewa mazoezi ya vitendo yanayokidhi mahitaji kwa sababu za
kiburi cha DVC-PFA. Katika jitihada za kutafuta waalimu wa ziada, DVC-ACR
amekataa katakata kutoa mwongozo wa kimaandishi ama ushauri wowote
utakaowasaidia viongozi wa CNMS kuboresha hali ya ufundishaji. Aliyekuwa Mkuu
wa Koleji ya CNMS anaweza kuonyesha nyaraka ambazo alizituma kwa viongozi hawa
wawili wa juu akiomba msaasda bila majibu. Kama kuna watu waliozembea katika
kazi hii ni DVC-ARC na DVC-PFA. Kwa mdomo, DVC-ARC alimshauri aliyekuwa Mkuu wa
CNMS atumie sera ya uzito wa kazi kutatua suala la uhaba wa waalimu. Hili
lisingaliwezekana.
4.
Sera ya Uzito wa Kazi (waorkload policy)
UDOM
imetengeneza sera ya uzito wa kazi (Workload Policy) ili kusimamia utekelezaji
wa utoaji wa taaluma ndani ya chuo. Sera hii ilitokana na; pamoja na mambo
mengine, usumbufu mkubwa ulioletwa na walimu wa muda (part time instructors)
kutoka vyuo vingine waliokuwa wanapewa mikataba ya kufundisha kuziba pengo la
uhaba wa walimu. Sera hii imesaidia sana kupunguza adha iliyokuwa inatokea
kabla ya kutengenezwa kwake. Sera hii imeeleza kwa uwazi wa namna ya kugawa
uzito wa kazi kwa kila mwanataaluma kama ifatavyo;
6 a.
Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant - TA) ambaye hana likizo ya masomo lazima
afundishe somo moja la diploma na kusimamia semina ya shahada. Akipangiwa somo
la ziada lazima alipwe
b.
Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant - TA) ambaye ana likizo ya masomo lazima
afundishe somo moja la diploma au cheti. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe
c.
Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer – AL) ambaye hana likizo ya masomo lazima
afundishe masomo mawili ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe
d.
Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer – AL) ambaye ana likizo ya masomo lazima afundishe
somo moja la shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe
e.
Mhadhiri (Lecturer), Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) na Profesa ambaye
hana majukumu ya madaraka lazima afundishe masomo matatu kuanzia ngazi ya
shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe.
f.
Mhadhiri (Lecturer), Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) na Profesa ambaye
ana majukumu ya madaraka lazima afundishe somo moja kuanzia ngazi ya shahada.
Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe.
g.
Ukubwa wa darasa (class size) itashughulikiwa na kila Koleji lakini
hairuhusiwi
kugawa darasa moja zaidi ya mara tatu hata kama lina wanafunzi zaidi ya 3000.
h.
Kuhusu mapato yatokanayo na programu zote ambazo si za shahada (Non degree
Programs), sera inatamka kwamba 70% ya mapato hayo yapelekwe kwenye Koleji
husika ili kuimarisha utoaji wa taaluma. 30% inabaki utawala mkuu kwa ajili ya
shughuli muhimu kama utoaji vyeti na mengine.
Tumeamua
kutaja sera hii ili kuonesha namna ambavyo isingewezekana kutumika
kushughulikia ufundishaji wa wanafunzi wa DE-SMICT ambao wanahitaji uangalizi
wa pekee. Hii itasaidia kuondoa upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu ndani
ya menejimenti ya UDOM kwamba Diploma husika inaweza kuhudumiwa kwa kutumia
sera hii. Limekuwepo jaribio kubwa la Menejimenti kulaz
imisha
jambo hilo
7
litokee kwa sababu wanataka kukumbatia mapato yanayotokana na Diploma hiyo huku
wakiwadhulumu wanafunzi na waalimu kwa KUKATAA KUANDAA
MAZINGIRA
MUAFAKA YA KUFANYA KAZI HII.
DVC-PFA
na DVC-ARC wanalazimisha sera hii itumike pale wanapotaka kukwepa jukumu la
kununua vifaa vya kufundishia, kukwepa kuwalipa waalimu na kulazimisha ULIPUAJI
KAZI. DVC-ARC na DVC-PFA hawataki kabisa kukumbuka sera hii inaafiki kutolewa
asilimia 70% ya mapato kwa Koleji husika.
5.
Mgogoro Uliosababisha Wanafunzi kutofundishwa
Kutok[truncated
by WhatsApp]
[5/30,
17:44] br kingu: Kutokana na maelezo yote hapo juu, jambo moja linajitokeza
hapa, Koleji zinazofundisha DE-SMICT zimezidiwa na kazi hasa CNMS na Koleji ya
Elimu (CoEd). Kutokana na kuzidiwa huko, hivi majuzi imeibuka mgogoro
uliopelekea wanafunzi kutofundishwa. Mgogoro huu unafana na ule wa kipindi cha
masomo cha mwaka 2014/15 uliopelekea SC kuundwa upya kama ambavyo nukuu mbili
zimewekwa hapo juu. Sisi chama cha wafanyakazi (THTU) tawi la UDOM, tunaamini
kwamba mgogoro huu umesababishwa na mambo yafuatayo;
5.1
Utamaduni wa bora liende unaolazimishwa na DVC-PFA pamoja na DVC-ARC
Katika
mgogoro huu, DVC ARC na DVC-PFA wamekataa katakata;
1.
Kununua vifaa vya maabara kwa ajili ya kufundisha waalimu hawa wa sayansi;
2.
Kuusaidia uongozi wa CNMS na CoEd kupata waalimu kwa idadi inayokidhi mahitaji;
3.
Kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuhakikisha kazi inafanyika katika ubora
unaowezekana na kukubalika;
4.
Kuwalipa waalimu kila inapotakiwa kufanya hivyo; Na;
5.
Kusema ukweli kwa Waziri, Katibu Mkuu na Watanzania kuhusu hali halisi ya
uendeshaji wa mafunzo haya.
8
Uzembe huu wa DVC-PFA na DVC-ARC pamoja na kiburi cha makusudi ndiyo chanzo cha
hali ilivyo hivi sasa ambapo takriban kwa WIKI TATU SASA WANAFUNZI HAWA WA
DE_SMICT WANAOCHUKUA MAFUNZO CNMS na CoED HWAJAINGIA MADARASANI.
Imedhihirika
pasipo shaka kwamba viongozi hawa wawili bila kujali uharabifu unatokea kwa
wanafunzi, chuo na Taifa kwa jumla wanapendelea utendaji kazi na utamaduni wa
BORA LIENDE pale wanapotakiwa kuwajibika.
Badala
ya kufanya kazi hii kwa ari, weledi na uaminifu kama ilivyostahili, viongozi
hawa wawili wameamua kuwa waongo, wasiojali maslahi ya wanafunzi na umma na
taasisi wanayoiongoza katika ujumla wake. Badala ya kushirikiana na wahusika
kutatua changamoto zinazojitokeza, wameamua kukaa ofisini na kutafuta suluhisho
kwa njia ya simu na kuandika barua. Kikubwa kinachokifanywa na DVC-ARC pamoja
na DVC-PFA ni kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wa Serikali waliojaribu kuingilia
hili swala ili kunusuru hali kwa kubambikia watu wasiowapenda makosa na kuanza
kushughulika nao badala ya kutatua taizo.
Ni
vema tukaweka kumbukumbu sahihi kwamba, Makamu Mkuu wa Chuo Prof
Idriss
Kikula tunamtoa katika hili. Tunaamini yeye binafsi angekuwepo, suala hili
lisingefika hapa tulipo sasa. Yapo matukio yanayoonesha kwamba tangu mwanzo wa
kudahiliwa wanafunzi, DVC-ARC na DVC-PFA hawajawahi kuwa na nia njema ya kuona
mambo yanakwenda vizuri. Baadhi ya mambo hayo ni
a.
Kumdanganya aliyekuwa waziri wa Elimu Dr. Shukuru Kawambwa kwamba vifaa vya
kutosha vipo wakati ni uongo mkubwa. Hili ni bora liende.
b.
Kudiriki kulazimisha Diploma hii maalum iingie kwenye mfumo wa kawaida ya
utoaji elimu wakati ilishaelezwa toka awali kwamba hii ni programu maalum, hili
pia ni bora liende.
c.
Kutokuwa tayari hata siku moja kukaa meza moja na walimu wanaofundisha masomo
hayo ili kufahamu tatizo la ziada. Badala yake wanamlazimisha Mkuu wa Koleji
kutatua mgogoro bila kumpa nyenzo, Bora liende linahusika
9 d.
Kukiuka makubaliano halali yaliyofikiwa ya kuunda kamati ya kushughulikia
mgogoro huu wakati Naibu Waziri Elimu na Katibu Mkuu walipokuja UDOM.
Menejimenti ya UDOM ilikataa majina yaliyopendekezwa na UDOMASA kuingia kwenye
kamati na kuwachagua watu wao inaowafahamu kuwakilisha UDOMASA. Hii peke yake
inaonesha dhahiri kwamba hawana chembe ya nia kutatua mgogoro isipokuwa bora
liende.
e.
Kusimamia misingi ya ubabe, vitisho, dharau na kutojali pale inapofuatwa na
viongozi wa UDOMASA na THTU kuangalia namna y atika mazingira hayohayo magumu
mpaka hali ilipoanza kubadilika.
6. Mazingira
magumu ya ufundishaji wa wanafunzi ambapo waalimu wamekuwa wanayalalamikia kwa
muda mrefu sana tangu program hii ilipoanza. Mgogoro huu umepotoshwa kutokana
na ukweli kwamba waalimu wanalazimika kufundisha historia ya sanyansi badala ya
sayansi kwa vitendo.Ukosefu wa nafasi na vifaa vya maabara ni tatizo kubwa
ambalo limelalamikiwa kwa muda mrefu lakini hoja inayoonekana zaidi ni malipo
ya waalimu. Mfano katika Chuo cha Sayansi Asilia na Mahesabu kinachohusika na
masomo ya Fizikia, Kemia, Baolojia na Hesabu maabara zake hazina vifaa vya
kutosha kukidhi mahitaji ya ufundishaji pamoja na koleji husika kutuma maombi
karibu kila mwaka.
Mapendekezo
ya ufumbuzi
UDOMASA tunaamini
kwamba kama Menejimenti ya chuo ingeonesha ushirikiano wa karibu kwa
waalimu wanaofundisha program hii na kushirikiana nao mambo haya yasingetokea
au yasingekuwa makubwa kiasi hiki hivyo tunapendekeza yafuatayo kufanywa ili
kuweza kutatua mgogoro huu
Kuwepo
mawasiliano na ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, Menejimenti ya chuo,
Menejimenti za Koleji husika na walimu.Kuangaliwa na kutatuliwa kwa changamoto
nyingine zilizoibuliwa na wanataaluma na wanafunzi katika uendeshaji wa program
hii badala ya kujikita kwenye suala la malipo tuSerikali kuwa na utaratibu wa
kuwasiliana na waalimu na wanafunzi mara kunapotokea matatizo vyuoni ili kupata
taarifa toshelezi toka pande zote.
IMETOLEWA
NA KAMATI TENDAJI YA UDOMASA
Tarehe 31/5/2016
Post a Comment