Mgodi wa dhahabu wa Geita umechangia
madawati 4,000 yenye thamani ya shilingi million 266 kwa Wilaya ya Geita.
Madawati hayo yatakayotolewa kwa
awamu mbili za mwaka wa masomo
yatapunguza adha kubwa inayowakabili wanafunzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo na
idadi kubwa ya wanafunzi walioandikishwa kwa mwaka wa masomo 2016 baada ya sera
ya Elimu bule kutangazwa.
Pamoja na uchangiaji wa madawati
,Halmashauri hiyo inauhaba wa vyumba vya 56 vya
madarasa,ikilinganishwa na uwiano wa wanafunzi kwa kila mkondo .
Mradi huo wa madawati ni moja ya shuguli
za kukuza uhusiano wa ujirani mwema kati ya jamii inayozunguka mgodi wa GGM
,ambapo tayari ujenzi wa karakana za uchomeleaji na mafunzo ya
utengenezaji wa matofali ya kisasa unaendelea mjini Geita.
Post a Comment