Wahamiaji 51 kutoka Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na Burundi wamekamatwa mkoani Kigoma wakiwa wameingia na
kuishi nchini kinyume cha sheria
Kamanda wa Polis Mkoa wa Kigoma
Fredinand Mtuhi amesema wahamiaji hao wamekamatwa katika msako mkali uliofanywa
na vyombo vya dola katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma.
Ameongeza kuwa katika operesheni
hiyo pia lita 302 za pombe haramu ya gongo zimekamatwa pamoja na debe tatu za
bangi.
Kamanda Mtuhi amesema watuhumiwa wa
uhamiaji na waliokamatwa na bangi na gongo
watafikishwa mahakamani wiki ijayo
baada ya uchuguzi kukamilika.
Post a Comment