MKOA wa KAGERA
umeshindwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JOHN
MAGUFULI kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu asiwepo mwanafunzi anayekaa
chini katika shule za msingi na sekondari kutokana na ukosefu wa madawati.
Kutokana na agizo hilo la Rais Magufuli alilolitoa wakati akiwaapisha wakuu wa
mikoa mapema mwaka huu, mkoa wa KAGERA ulipaswa kutengeneza madawati
73,874 ili kutimizia mahitaji ya madawati 200,439.
Madawati yaliyopaswa kutengenezwa yanajumuisha ya shule za msingi 64,601 na
sekondari 9,273, lakini yaliyotengenezwa ni 35,956 yakiwamo ya shule za msingi
30,960 na ya sekondari 4,996. Upungufu uliopo sasa ni madawati 37,918.
Kufuatia jitihada zilizofanywa na serikali za kuhakikisha madawati yanayopungua
yanataengenezwa, mkuu wa mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu SALUMU MUSTAPHA
KIJUU amewapongeza wananchi wote mkoani hapa, taasisi za serikali
na binafsi na makampuni yaliyoguswa na kuchangia madawati hayo.
Aidha ameendelea kuhamasisha kila mwananchi au taasisi itakayoguswa na suala
hili la uchangiaji wa madawati kuendelea kuchangia, ili tumalize tatizo la
watoto kukaa chini, na kuwawezesha kupata elimu bora katika mazingira rafiki
ya kujifunzia.
Ametaja baadhi ya changamoto zilizochangia kutokamilika kwa utengenezaji
wa madawati kwa wakati kuwa ni pamoja na kuwapo kwa tafsiri duni ya dhana ya
elimu bila malipo na kufanya wananchi mwanzoni kuanza kusuasua kuchangia.
Changamoto nyingine ni kutumia muda mwingi kusubiri mbao kukauka na kutokuwa na
umeme wa uhakika kwani madawati mengi yanatengenezwa kwa fremu za chuma katika
wilaya ya Ngara, na kuwa halmashauri ambazo bado hazijakamilisha, zitakamilisha
zoezi hilo kabla ya Julai 30 mwaka huu.
Hata hivyo katika utengenezaji huo, manispaa ya Bukoba imevuka lengo kwa
kutengeneza madawati 244 ya ziada, na kufanya yaliyopo sasa kufikia 8,776
badala ya 8,532 yaliyohitajika.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment