Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: LOWASSA AUDHURIA TUKIO LA KUWEKWA WAKFU ASKOFU JACKSON NASOORE NAIROBI, KENYA.
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Leo tarehe 3 julai Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward N Lowassa alikua moja wa wageni waalikwa sambamba na Rais wa Jamuhuri ya Ken...
 
Leo tarehe 3 julai Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward N Lowassa alikua moja wa wageni waalikwa sambamba na Rais wa Jamuhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta, katika tukio kubwa la kumuwekea wakfu Askofu wa jimbo kuu la kanisa la Anglikana Kenya, Askofu Dr. Jackson Nasoore Ole Sapit iliyo fanyika kwenye kanisa la "All Saints Cathedral Nairobi".

 
Ni miezi michache imepita tuliposhuhudia Magufuli Akimkaribisha nyumbani kwake Chato Raila Odinga, waziri mkuu mstaafu wa Kenya. Ni kiongozi wa kwanza aliyekaribishwa na Magufuli katika East afrika hapa Tanzania.

Leo Lowassa kakaribishwa Kenya kuhudhuria kusimikwa kwa Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini humo. Tunajua Lowassa ni Mlutheri, sasa sijajua kaalikwa kama nani!!

Kwa mtazamo wangu mualiko wa Lowassa ni kama wa kisiasa zaidi, na inawezakua hii ni sababu iliyotumika kwa yeye kuweza kuonana na Kenyata.

Odinga ni Waziri mkuu mstaafu, alikihama chama chake cha Kanu kilicho mlea na sasa yupo ODM, Lowassa nae ni waziri mkuu mstaafu, alikihama chama chake cha CCM na sasa yupo Chadema.

Wote hawa wanautaka Urais katika nchi zao. Magufuli Rafiki yake ni Odinga, na atafurahi pale ambapo Odinga akifanikiwa kuwa Rais wa Kenya, Kenyata nae Rafiki yake ni Lowassa, nae hivyohivyo akiwa Rais wa Tanzania.

Odinga akiwa Rais wa Kenya, nafikiri ndio mwisho wa Kenyata kwenye Siasa.
 Je Kenyata nae akifanikiwa kuwa Rais wa Kenya kwa mara ya pili, kwa upande wa lowassa itakuajee 2020??










About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top