Wananchi wa kata ya Mabira wilayani Kyerwa mkoani Kagera
wametakiwa kuzingatia agizo la serikali la kutengeneza vyoo bora ili kuepuka
mlipuko wa magonjwa yanayotokana na uchafu.
Wito huo umetolewa na afisa afya wa kata ya Mabira
Jackiline Shukuru Gamale wakati akiongea na watendaji wa vijiji,wenyeviti wa
vijiji na wahudumu wa afya wa vijiji kuhusu taarifa ya ujenzi wa vyoo bora
katika kata hiyo.
Amesema kuwa kila familia inatakiwa kujenga choo bora kwa
kutumia saluji hivyo ni jukumu la viongozi kuhakikisha wanahamasisha wananchi
wote kuwa na vyoo vya namna hiyo kabla ya muda uliopangwa kufika.
Amesema kuwa ujenzi wa choo bora ni afya ya kila mmoja
hivyo nguvu ya serikali itatumika kwa wale ambao watakaidi kufuata agizo hilo.
Gamale amezungumzia pia suala la usafi kwa ujumla
akisisitiza kuwa ni la kila siku na sio kusubiri siku ya alhamisi au jumamosi
ya kila mwisho wa mwezi.
Post a Comment