Watanzania wameaswa kujielimisha ili
kushiriki kikamilifu katika kufanikisha mpango wa maendeleo Endelevu ambao unalenga kuikwamua nchi katika umaskini
na kukuza uchumi.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa
kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama wakati akizungumza na MTANDAO HUUkwa lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea banda la Umoja wa Mataifa
(UN) katika maonesho ya 40 ya Biashara Jijini Dar es salaam na kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu
SDGs pia kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.
Aidha Usia Nkoma ameeleza lengo la UN kuwepo katika
Maoneosho hayo ya Biashara.
Katika kuelekea kilele cha Maonyesho
ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa
Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar akiwa
mgeni wa kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka zake kwenye
maonyesho hayo.
Amapo Nkoma amepongeza hatua ya
kiongozi huyo na kuwahamasisha viongozi wengine kuiga mfano wake kwenda kuvuna
maarifa kutoka umoja wa mataifa UN kwa ajili ya elimu kwa wananchi wake.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kujenga
mahusiano mazuri na umoja huo sambamba na kuwa Karibu nalo ili waweze
kujikwamua kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni kwani shirika hilo
limekuwa likijikita katika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
jamii.
Post a Comment