Wazazi na walezi katika manispaa
ya BUKOBA mkoani KAGERA wameshauriwa kutambua umuhimu kuwanyonyesha watoto wao
maziwa ya mama katika kipindi cha miezi sita hadi miaka miwili ili
kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima..
Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa manispaa ya bukoba DK HAMZA MUGULA wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa FADECO Radio juu ya umuhimu wa kumunyonyesha mtoto .
DK MUGULA ametoa kauli hiyo zikiwa zimebaki siku chache kabla ya maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji nchini.
Amewataka wazazi kutambua kuwa maziwa ya mama ni muhimu hususani kwa watoto katika kipindi cha miezi sita kwani maziwa hayo yanavirutubisho ambavyo vinazuia magonjwa mbalimbali kwa mtoto.
DK MUGULA amezitaja changamoto zinazokabili khali ya lishe kuwa ni kuamini mila na destuli potofu watoto kuachishwa kunyonyeshwa mapema pamoja na huelewa mdogo kuhusu maswala unyonyeshaji.
Hata hivyo katika kukabiliana na changamoto hizo DK MUGULA amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu ya unyonyeshaji na lishe kwa watoto wadogo pamoja na chakula kinachotakiwa kwa wanawake wenye ujauzito na wenye watoto wachanga .

Post a Comment