NAIBU waziri wa elimu sayansi na teknolojia mhandisi Stella
Manyanya ameahidi kujenga bweni moja la kisasa na kutoa vitanda 100 katika
shule ya sekondari Bugene ambayo ina kidato cha tano na sita.
Hayo yalisemwa
jana na mhandisi manyanya alipokuwa katika chuo cha ufundi cha halmashauri ya
wilaya ya karagwe,Karagwe District Vocational Training Center (KDVTC) baada ya
kupokea taarifa ya elimu ya wilaya ya karagwe na kukagua miundombinu ya chuo
hicho.
“Niliwahaidi tu kwamba
tayari wizara imejikomiti kujenga bweni zuri la kisasa na kuweka vitanda 100
katika bweni hilo ili kuongeza molali kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya
Bugene lakini pia ikizingatiwa kwamba wilaya hii ipo mpakani na shule za nchi
hizo ni nzuri ”alisema mhandisi Manyanya
Akisoma taarifa ya
wilaya afisa elimu sekondari wilaya ya karagwe Upendo Rweyemamu alisema kuwa
halimashauri ya wilaya hiyo ina shule moja ya sekondari ya Bugene ambayo ina
kidato cha sita.kati ya shule 25 za sekondari za serikali na inachangamoto
mbalimbali ikiwemo pamoja na upungufu wa mabweni ya wasichana na wavulana
na vitanda vipatavyo 120.
Rweyemamu
alieleza kuwa halimashauri ililenga kupokea wanafunzi 90 ikiwa ni wavulana 45
na wasichana 45 kidato cha tano katika shule ya Bugene na kwamba waliopangwa
walikuwa 160 wakiwemo wavulana 80 na wasichana 80 hadi tarehe 5 agosti mwaka
huu walikuwa wamepokelewa wanafunzi 125,wavulana 66 na wasichana 59.
Alitaja hali ya miundo
iliyopo shuleni hapo kuwa ni pamoja na bweni moja la wavulana na bweni
moja la wasichana ,umeme,bwalo na vyumba vya madarasa changamoto nyingine
alizitaja kuwa ni vitanda 120 na vitanda 30 viliazimwa kutoka kituo cha afya
kayanga na vitanda 60 vimeanza kutengenezwa.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya karagwe Walles Mashanda
alimpongeza naibu waziri kwa kitendo chake cha kuonyesha nia ya kujenga bweni
la kisasa na vitanda katika shule hiyo huku akimuomba kuongezewa walimu katika
shule za msingi kwa kuwa wilaya hiyo ina upungufu wa walimu 834 na mwaka jana
walipata walimu saba tu!.
Aidha Mashanda
alimuomba mhandisi Stella manyanya kutatua changamoto ya walimu wa sayansi
kwani halimashauri ya wilaya ya karagwe inakabiliwa na upungufu wa walimu
wapatao 87,ambapo alisema kuwa wilaya inahitaji walimu wa sayansi wapatao 169
na waliopo ni 82.
Post a Comment