WATUMISHI wa idara ya mahakama wilayani karagwe mkoani Kagera wametakiwa
kuepuka vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa wananchi wenye malalamiko yao ili
kujenga imani ya chombo hicho kwa jamii.
Hayo yalibainishwa jana
na mtendaji wa mahakama kuu kanda ya Bukoba Ignosia Kabale katika
semina ya mpango mkakati wa mahakama ya Tanzania wa miaka mitano kuanzia 2015
hadi 2020 unao lenga kufikia malengo kwa watu wote, utawala bora, kurejesha
imani ya mahakama kwa jamii pamoja na ushirikishwaji wa wadau katika kazi
za mahakama iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama hiyo.
Kwa mjibu
wa mtendaji huyo aliye wakutanisha watumishi wa mahakama hiyo alisema kuwa
katika kuhakikisha mpango huo unatimizwa ni vyema watumishi wa idara ya
mahakama wilayani karagwe kuhakikisha wanaepuka vitendo vya kupokea rushwa
kutoka kwa wanachi wenye malalamiko Yao kwani siyo maadili kwa watumishi wa
mahakama.
Alisema kuwa tatizo la rushwa
limekuwa changamoto kubwa ya kushughulikia matatizo ya wananchi na kufanya
chombo hicho kukosa imani kwa jamii suala ambalo haliwezi kujenga heshima
kwa watumishi.
Naye mhasibu mkuu wa mahakama ya Tanzania
Fanuel Tiibuza alisema kuwa suala la kutoa lugha chafu kwa wateja wa mahakama
imepelekea baadhi ya malalamiko kutoshughulikiwa kwa wakati muafaka hususani
katika maeneo ya vijijini ambapo baadhi ya wanachi hawajui haki zao zinazo
paswa kutolewa na mahakama.
“Utakuta mwananchi ana
malalamiko yake anakalishwa kwa muda mrefu na karani bila kushughulikiwa wakati
mwingine hutolewa lugha chafu pasipo kumuhudumia shida yake na kumpiga tareha
“Alisema Tiibuza.
Aidha katika
kuhakikisha mpango mkakati huo unatimizwa Naibu Msajili mahakama kuu ya kanda
ya Bukoba Seif Kulita alikabidhi vitabu 10 vya mwongozo wa ukaguzi wa mahakama
namba za simu nchini kote Tanzania bara ofisi za mikoa na wilaya na mahakama
zote,mabango kwa ajili ya elimu na utoaji taarifa,malalamiko,maoni,ushauri au
pongezi kwa mahakama hiyo.
Hata hivyo hakimu
mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Paul Magoryo alishukuru kwa semina hiyo na
kuwataka watumishi wa idara ya mahakama kuhakikisha wanayafanyia kazi maagizo
hayo ikiwa ni pamoja na kutenda kazi kwa weledi wa utumishi wa umma.
Post a Comment