Serikali ya Mkoa wa Kagera
leo Septemba 14, 2016 tayari imepokea misaada mbalimabli ya fedha taslimu na
mahitaji mbalimbali kama Sukari, Mchele, Unga, Maji ya kunywa, Sabuni,
Blanketi, Shuka Maharage, matrubali, Mbao na Sementi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
32.
Aidha, Kamati ya Maafa ya
Mkoa tayari imeanza kugawa mahitaji hayo kwa wananchi waliopatwa na janga la
tetemeko na kwa sasa hawana mahala pa kuishi. Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa
Kashabo Manispaa ya Bukoba wamegawiwa mahita ji hayo na aliyeongo zoezi hilo ni
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe, Meja Jenerali Mstaafu Salim M. Kijuu ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa.
Katika hatua nyingine Kamati
ya Maafa ua Mkoa imeamua kutoa bati 20 na sementi mifuko 5 kwa kila mwananchi
ambaye nyumba yake ilianguka kabisa au haifai kuishi tena. Aidha, wapangaji waliokuwa wanapanga katika
nyumba hizo watalipiwa kodi ya miezi na Serikali sita kila mwezi 20,000/=
Katika hatua nyingine Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu ameandaa kikao cha harambee ya kuchangia maafa
mkoani Kagera tarehe 16.09.2016 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa kuanzia saa 3:00 Asubuhi na
anawaalika wadau wote kuja kuchangia katika harambee hiyo.
Aidha kwa wale wanaotaka
kuchangia lakini hawatahudhuria wanaweza kuchangia kupitia Akaunti ya Benki
iliyopo CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti
Namba. 0152225617300. Tunawashukuru wote wanaoendelea kuchangia na Mungu
awazidishie.
Imetolewa
na: Sylvester M. Raphael
Afisa Habari (Mkoa )
KAGERA
Septemba
14,2016
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
- MKUU WA MKOA KAGERA AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUFIKISHWA OFISINI KWAKE AKIWA NA PINGU MIKONONI BAADA YA KUITIA SERIKALI HASARA08 Mar 20180
Na Sylvester Raphael Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampun...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.