RAIS
John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa majeshi ya
ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo
baada ya kutimiza umri kwa mujibu wa katiba na sheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo Upanga jijini Dar es
salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia
wanne wa Jeshi la ulinzi nchini pamoja na Meneja Jenerali wawili
ambapo wote kwa pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria
ya jeshi hilo.
“Mimi
mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais
na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka
mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe 31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange
Jeneral
Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo
imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .
Hata
hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua Luteni
Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la
wananchi.
Sanajari
na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia Rais Magufuli amefanya uteuzi
mkubwa ndani ya Jeshi hilo kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya jeshi
hilo.
Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais ni Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa
kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu ambaye amechukua nafasi ya
meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya
kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni
mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.
Jeneral Mwamunyange alimtaja pia kamanda mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi
kuwa Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) kuchukua nafasi
ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu
mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii. Meja Jenerali Sirakwi alikuwa
mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.
Mwingine aliyeteuliwa na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali George William Ingram
kuwa Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga ambaye anachukua nafasi ya Meja
Jenerali Joseph Pwani aliyestaafu leo kisheria baada ya kufikisha
umri wa kustaafu. Bregedua Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika
mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.
Pia Rais Magufuli amemteua Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo
kuwa Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali
Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo,baada ya kufikisha umri wa kustaafu
kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao
mkuu ya jeshi.
Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu
kuwa mkuu wa shirika la mizinga kuchukua nafasi ya Meja Jenerali
Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umri
.Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao
mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.
Pia Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjela
kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS) kuchukua nafasi ya Brigedia
Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi baada ya kufikisha umri wa kustaafu
kisheria .Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa
Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Aidha,Rais Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole
kuwa Kamanda wa Brigedia ya Tembo kuchukua nafasi ya Brigedia
Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo kisheria baada ya kufikisha
umri wa kustaafu,.Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa
Afisa Mnadhimu makao makuu ya Jeshii.
Rais Magufulia pia amemteua Bregedia Jenerali Sylevesta M.Minja
kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda kuchukua nafasi ya Meja Jenerali
Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa
kustaafu kisheria ambapo kabla ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa
mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.
Post a Comment