Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: ATUKUZWE FC NAYO YAANZA LIGI KWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Timu    ya    Kamachumu    Fc   kutoka   wilayani   Muleba   imejipatia   mshindi    wa   magoli   3-1   dhidi   ya   Atukuzwe   Fc ...
 
Timu   ya   Kamachumu   Fc  kutoka  wilayani  Muleba  imejipatia  mshindi   wa  magoli  3-1  dhidi  ya  Atukuzwe  Fc  ambao  ni  wenyeji  wa    wilaya  ya  Karagwe  katika  mchezo   wa  ligi  ya  Taifa  mkoa  wa  Kagera  ambayo  inaendelea  kwa  kituo  cha  Karagwe moani  Kagera.

Timu  ya   Kamachumu  Fc  ilikuwa  ya  kwanza  kujipatia  goli  dakika  ya 3 kupitia  kwa  mshambuliaji  wa Joseph Mashoto baada  ya  beki  wa  mwisho  wa  Atukuzwe  Ayoub Meshack  kuteleza  na  mshambuliaji  huyo  kuwahi  mpira  na  kuachia  shuti  kali  lililomshinda  mlinda  mlango  Sadock  Babwanga.

Atukuzwe  Fc  waliongeza  kasi  ya  mashambulizi  na  kufanikiwa  kusawazisha  goli  hilo  dakika  18  baada  ya mabeki  wa  Timu  ya  Kamachumu  Fc   kushindwa  kuondoa  mpira  langoni  mwao  ambapo  ilikuwa  piga  ni  kupige    ndipo  mchezaji  wa  Atukuzwe  Fc   Ibrahimu  Mbwilo   Alipata  nafasi  ya  kumalizia  mpira  huo.



Mchezaji  huyo   Ibrahimu  Mbwilo  alisema  kilichowapelekea  kupoteza  mchezo  huo ni  kutokana  na  wachezaji  wenzake  kutojipanga  vizuri.



Kamachumu  Fc  walijipatia  bao  la  pili    dakika  38  kupitia  kwa  mshambuliaji  Kayana  Kaiza baada  ya  kuwahi  mpira  uliowashinda  mabeki  wa  Atukuzwe   kuuondoa  katika  eneo  la  hatari  hadi  mapumziko  Kamachumu  Fc  goli  2  na  Atukuzwe  goli  1




Kipindi  cha  pili  kilianza  kwa  kasi kwa  timu zote  kufanya  mashambulizi  ya  mara  kwa  mara   ilikuwa  ni  Kamachumu  Fc iliyoweza  kujiongezea  goli  na  kujihakikishia ushindi  dakika  65 kupitia  kwa  mchezaji Kayana  Kaizaaliyepokea  mpira  kutoka  wingi  ya  kulia  na  kumkuta  katika  nafasi  nzuri  ya  kufunga.



Emanueli  Byarufu  ambaye  ni  kocha  wa  timu  ya  Atukuzwe  alisema  maandalizi  yalikuwa  ni  hafifu  na  kuongeza  ilikuwa  ni  kukurupuka  hivyo  akasema  anajipanga  kwa  ajili  ya  mechi  ijayo.

Katika  mchezo  ulioanza  majira  ya  saa  nane  mchana  uliozikutanisha  timu  ya  Benaco  stars ya  wilaya  ya  Ngara   na  Chandimu   stars  kutoka  Manispaa  ya   Bukoba ilishuhudi  timu  ya  Chandimu  ikijipatia  ushindi  wa goli  2-1  Benaco   ndio  walikuwa  wa  kwanza  kujipatia  goli  dakika  ya 10  ya  kipindi  cha  kwanza  kupitia  kwa   Athuman   Nuru




Kuingia  kwa  goli  hilo  kuliwaamusha  wachezaji  wa  timu  ya  Chandimu  wakaanzisha  mashambulizi  ya  mara  kwa  mara  langoni  mwa  Benaco  Stars  na  kufanikiwa  kusawazisha  goli  hilo   dakika 35  ya  kipindi  cha  kwanza  na  mfungaji  akiwa  ni Evodius   Kapilipili
Chandimu  ilijipatia  goli  la  ushindi  dakika  za  lala salama  dakika  88  ya  mchezo  kupitia  kwa  mchezaji   wao    Fidel  Fidelisi    akitumia  makosa  ya  mlinda  mlango  aliyetoka  langoni  kuwahi  mpira  bila  ya  kuwasiliana  na  mabeki  wake.



Makochi  wa  timu  zote  wamezungumzia  mchezo  huo  na  ligi  kwa  ujumla  wakisema waamuzi  kuwa  wametenda  haki  na  kuongeza  kuwa  kiwanja  bado  kwao  ni  tatizo  kwani  hawajauzoea  lakini  kwasababu  wameishaingia  vitani  hamna  haja  ya  kuogopa.
Emanueli  Byarufu  ambaye  ni  kocha  wa  timu  ya  Atukuzwe  alisema  maandalizi  yalikuwa  ni  hafifu  na  kuongeza  ilikuwa  ni  kukurupuka  hivyo  akasema  anajipanga  kwa  ajili  ya  mechi  ijayo.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top