Serikali imekiri kuwepo kasoro
nyingi zilizojitokeza katika mradi Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
unaotekelezwa na TASAF ikiwamo ubadhirifu wa fedha kwa Kaya sizizokuwa na sifa
kupewa pesa kupitia mpango huo hivyo imejipanga kuborsha zaidi mpango huo
katika awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya
zinazolengwa.
Akijibu swali la Magdalena Hamisi
Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa
Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru
Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa
kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.
Amesema Wakusanya taarifa
huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia
nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na
mkutano wa Kijiji ila bado kuna malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini
zinaachwa na kupewa Kaya nyingine ambazo sio maskini
Waziri Kairuki amesema Mpaka sasa
kutokana na malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini
zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewawajibisha watendaji toka kijiji cha
Kibondo Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, na Kigoma.
Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza
kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni
fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zinatolewa na
Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza
kupata Elimu Malazi na chakula bora.
TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya
maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha
Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.
Post a Comment