JAJI
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othuman ametoa siku saba kwa mahakimu
508 watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na
kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.
Jaji
Mkuu Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa
habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni
sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.
Alisema
kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na
Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama
hizo wameamua kesi chini 100 mwaka jana.
Alibainisha
kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo
mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi
chini ya 100 mwaka jana.
"Ukiondoa
wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za
mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliokwenda masomoni katikati ya
mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.
"Majaji
Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuainisha mahakimu wote walioshindwa
kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa
mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini
wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande
Jaji
Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka
idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane
ni hatua gani wanachukuliwe.
"Mahakama
haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya
hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika
mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini
ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo," alisema
Jaji
Mkuu Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa
hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na
kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.
"Mahakimu
wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoa
sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko
walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za
Mahakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," alisema
Hata
hivyo, Jaji Mkuu Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka
kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na
mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.
Alisema
mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna
baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka
upya.
Jaji
Mkuu Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi
34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha
kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 ni
zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji
asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.
Post a Comment