Mbunge
wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma)
ameishauri serikali kuruhusu kisheria kilimo cha Bhangi na Mirungi
ili kuiwezesha kujipatia fedha za kigeni kutokana na mauzo ya
mazao hao
Mbunge
huyo aliyasema hayo jana katika kikao cha 5 cha bunge la 11
linaoendelea na vikao vyake katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu .Mfano
mzuri mfano ni majirani zetu wa Kenya ambao ndege mbili kubwa hutua
nchini humo kuchukua mirungi na kupeleka ulaya,sasa kwa nini sisi
tusiendeleze zao hili linalopatikana Geita na maeneo ya Bunda mkoani
Mara na maeneo mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa kuuza zao hilo
?'' Alihoji Msukuma na kuongeza;
"Kwa
wasukuma kule kwetu mtu akitumia bhangi anapata nguvu ya kulima sana
hata hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo huo vijana wetu
tumewaruhusu kutumia viroba ambavyo huwadhoofisha sana pengine kushinda
hata bhangi, naomba tufanye utafiti upya juu ya hili.
"Wapo wenzetu humu (wabunge) wanaitumia bhangi na hakuna madhara yoyote, tena wanachangia hoja kwa ufasaha kabisa."
Baada ya hoja hiyo ya Mbunge Msukuma, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt Khamis Kigwangalla alisimama kumjibu ambapo alisema madawa ya
kulevya aina ya bhangi na mirungi yana athari kubwa sana za kiafya na
hasa afya ya ubongo .
Kingwangalla alisema serikali kwa namna yoyote haitakubali kuruhusu au kujadili kuhalalishwa kwa madawa hayo.
Post a Comment