Wizara ya afya, jinsia ,wazee na watoto kwa kushirikiana
na mpango wa wa taifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele inategemea kufanya
kampeni ya utoaji wa dawa za kinga kwa watoto walio na umri kati ya miaka
mitano hadi kumi na tano.
Hayo
yamebainishwa leo katika
kikao kilichofanyika katika
ofisi ya mkuu
wa wilaya ya
Karagwe kilichokuwa na
lengo la kujadili mikakati ya
kufanikisaha zoezi la
utoaji chanjo kwa
magonjwa yasiyopewa kipaombele kwenye
jamii.
Katibu Tawala wa
wilaya ya Karagwe
Mustafa Said amesema
kuwa ni muhimu
wazazi, walezi na jamii
kwa ujumla kutoa
ushirikiano katika zoezi
hillo muhimu la
kutoa chanjo ili
kupunguza magonjwa hayo
kwani husababisha watoto
kuacha masomo yao.
Amesema kuwa zoezi
hilo la utoaji
chanjo litafanyika katika
kanda 16 zilizopo
nkwenye wilaya ya
Karagwe na kuongeza
kuwa ili watoto
wasipate madhara ya
dawa hizo ni wajibu
wa wazazi,walezi pamoja
na kamati za
shule kuhakikisha kuwa
chakula kinapatikana kabla
ya kutumia dawa
hizo.
Kaimu Mganga Mkuu
wa wilaya ya
Karagwe Ezikeli Bulyana
amesema serikali imetoa
kiasi cha shilingi 100,000 kwa
ajili ya kusaidia
shule kupata kianzio
cha kuwapatia chakula
waqnafunzi lakini
akabainisha kuwa kiasi
hicho halkitoshi hivyo
kamati za shule,wazazi
na walezi hawana
budi kuongeza nguvu
zao kwa kuchangia
ili kutosheleza mahitaji
na kufikia lengo.
Hata hivyo wamebainisha
magonjwa hayo yasiyopewa
kipaombele ni
Kichocho,Minyoo ya tumbo, Matende na Mabusha
au Ngirimaji.
Post a Comment