Jeshi la polisi mkoani KAGERA linamshikilia mfanyabiashara mmoja
wa manispaa ya BUKOBA mkazi wa kata Rwamishenye kwa kuhifadhi sukari tani mbili
huku wananchi wakiwa wanaendelea kukosa
sukari katika maeneo mbalimbali
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA AGUSTIN
OLLOMI amemtaja anayeshikiliwa ni BENEDICTO BUCHARD ambaye alikuwa ana mifuko
80.
Amebainisha kuwa mtu anayefanya hivyo anawanyanyasa wananchi wenzake
ikiwa wanakosa sukari madukani huku yeye akificha sukari ili awauze kwa gharama
ya juu.
Katika hatua nyingine mfanyabiashara huyo amekamatwa na pombe
haramu aina ya viroba ambavyo vimezuiliwa kuingizwa nchini.
Kwa mujibu wa kamanda OLLOMI amesema kuwa pombe hizo zinatoka nje
ya nchi na mfanyabiashara huyo ameingiza pombe hizo kinyume na sheria.
Post a Comment