Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZAZI NA WALEZI WENYE WATOTO WENYE UALIBINO WATAKIWA KUWAONESHA UPENDO WATOTO WAO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wazazi,walezi  na  jamiii  kwa  ujumla  wametakiwa  kutimiza  wajibu  wao  wa  kuwatunza  na  kuwalea  watoto  wenye  ulemavu   na ...


Wazazi,walezi  na  jamiii  kwa  ujumla  wametakiwa  kutimiza  wajibu  wao  wa  kuwatunza  na  kuwalea  watoto  wenye  ulemavu   na  wasiokuwa  na  ulemavu  kuliko  kuachia  jukumu  hilo  serikali  pekee  kwani  ni  jukumu  lao  wote.

Kauli  hiyo  ilitolewa  jana  na  Katibu  Tawala  wa  wilaya  ya  Misungwi  Elius  Nyakia  wakati  akitoa  hotuba  kwa  wana  warsha  ya  kufanya  tathimini  ya  mpango  mkakati  wa  kutoa  elimu  juu  ya  kuzuia  ukatili  na  unyanyasaji  kwa  watu  wenye  ualibino  ambayo  imejumuisha  maafisa  maendeleo  ya  wilaya   na  mikoa  ,wanahabari,watu  wenye  ualibino ,walimu  wa  shule  za  Buhangija  ,Mitindo  pamoja  na  askari  wa  madawati  ya  jinsia.

Alisema  wazazi,walezi  wenye  watoto  wenye  ualibino  wamekuwa  nma  tabia  ya  kuwatelekeza  kwenye  shule  ya  Mitindo  ambayo  inapokea watoto  wenye  ualibino  na  ulemavu  mwingine  ukiwemo  wasioona  alisema  wakishawafikisha  hakuna  mawasiliano  wala  kutoa  matumizi  jambo  ambalo   linachangia  mzigo  kuwa  mkubwa  kwa  serikali    katika  kuwahudumia  watoto  hao.


“Jamani  wana  warsha  mnapojadili    jikiteni  kutoa  elimu  kwa  wananchi  wabadili  imani potofu  za  kiufikiria  kuzaa  mtoto  mwenye  ualibino  au  ulemavu  wa  aina  yoyote  ile  ni   mkosi  kwa  familia ,hata  wanasiasa  nao  ni  tatizo  juzi juzi diwani  mmoja  alituletea  mtoto  mwenye miezi  mitatu  kweli  inaingia  akilini  “Alihoji  Nyakia

Wana  warsha  hiyo  ya  siku  tatu  walitembelea  shule  ya  Mitindo  iliyopo  wilayani  Misungwi  na  kujionea  na  kuongea  na  wanafunzi  wenye  ualibino  na  wengine  ambao  wana  ulemavu  tofauti  ambao  jumla  yao  ni  2016  waliopo  shuleni  hapo.

Mwalimu  Mika  Sholla  ambaye  ni  mwalimu  katika  shule  ya  Mitindo  pia  ni  mlemavu  wa  asiyeoona    aliwataka  wanaharakati ,waandishi  wa  habari  kuahikikisha  wanatumia  nafasi  zao  kuwatetea  watu  wenye  ulemavu    kupata  walau  elimu  ya  ujasriamali  kwani  siyo  wote  wana  uwezo  wa  kwenda  shule  na  wengine  tayari  wameishavuka  umri  wa  kuanza  shule.

Mwalimu  Mkuu  wa  shule  ya  Mitindo  Kulwa  Mghwelo  alisema  shule  hiyo iliyoanzishwa mwaka  1956   ina  jumla  ya  wanafunzi  1357  kati  yao  wenye  ulemavu  ni 2016   katika  mchanganuo  ufuatao   Viziwi 40,Ualibino 86,Wasioona 34,uoni  hafifu 20


Alisema  changamoto  kubwa  ni wazazi  na  jamii  kwa  ujumla   kutoona  umuhimu  wa  kutoa  upendo  na  matunzo  kwa  wanafunzi  hao  hata  kuwatembelea  zaidi  wanaendesha  kwa  kutegemea  nguvu  ya  serikali  na  wahisani  wachache  wanaojitokeza.

Mwanafunzi  Juma  Marco  ambaye  ni  mwenye  ualibino  alinusurika   kuwawa  kwenye  tukio  ambalo  alipoteza  mama  yake  mzazi  alisema  anatamani  kuwa  na  familia  yake  akiwa  huru  kuliko  ilivyo  sasa  wanalindwa  na  askari  usiku  na  mchana  kushinda   askari  mgambo  kuwa  angelitamani  siku  moja  kuwa  huru  na  ndugu,majirana  na  familia  yake.

Afisa  Maendeleo  ya  wilaya  ya  Misungwi   Aliadina  Peter  ambaye  ni  mwanawarsha  alisema  wilayani  kwake  wapo  watoto  wenye  ualibino  129 ambapo  wavulana 61 wasichana 68  na  watu  wazima  wapo  22 kwa  wilaya  nzima.


Aidha amewahakikishia usalama wa wanafunzi wenye ualbino na kwamba Pamoja na masomo mengine wanatoa pia Elimu ya ufundi selemara, Computer na Ushonaji.


Ametaja changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kuwa ni wazazi kutotoa ushirikiano katika malezi ya watoto wao hasa wenye ualbino kwa kwenda kuwatembelea shuleni hapo wakifikiri kuwa kazi ya malezi ni ya walimu na serikali.


Kwa mujibu wa mwalimu Mkuu Kulwa Nghwelo shule hiyo ilianza mwaka 1956 ina walimu 50, matroni 2 na Patroni 2 ambapo inapokea wanafunzi kuanzia darasa la awali na kuwa Idadi kubwa ya  wanafunzi  wanaoletwa shuleni hapo wanatokea wilaya za Kwimba, Sengerema, Geita, Ukerewe na wachache kutoka katika Wilaya nyingine.
 
washiriki wa warsha wametoa zawadi kwa watoto wa shule ya  Msingi Mitindo yenye wanafunzi jumuishi kwa watoto wenye ulemavu wa aina tofauti na wasio walemavu, ambavyo ni Box za biscuit, Jwice, Sabuni na pipi vyenye thamani ya shilingi laki tatu na ElfuTisini(390,000).






Hata  hivyo  wanawarsha  hiyo  walisema  kuwa   elimu  zaidi  inahitajika  kuendelea  kutolewa  kwani  jambo  la  kumbadilisha  mtu  imani  siyo  la  siku  moja  au  la  dharula  kama  ugonjwa  wa  kipindupindu.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top