Wadau
wa mazingira kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe
mkoani Kagera wameweka mikakati ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yenye vipara
ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wakiongea
na viongozi ngazi ya vijiji na kata za Nyakakika,Nyakabanga,Kibondo, na
Nyabiyonza wamesema kuwa mabadiliko
makubwa ya tabia ya nchi yanasababishwa na vitendo na shughuli za binadamu.
Mratibu
wa mradi wa utunzaji wa mazingira wa Kanisa La Kiinjili la Kiruthel Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Karagwe Horace Kamkoto
ametaja baadhi ya shughuli za binadamu zinazochangia uharibifu wa
mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Afisa
kilimo wilaya ya Karagwe Cleophace Kanjagaire ameeleza kuwa kilimo kisichofuata
utaratibu wa kitaalam nayo ni sababu inayosababisha katika uharibifu wa
mazingira.
Mojawapo
ya mikakati iliyowekwa na wadau hao ni pamoja na kupanda miti kwa wingi katika
vilima vyote vilivyo wazi,kuacha tabia ya kuchoma moto ovyo,na kufuata ushauri
wa wataalam katika kulima na kufuga.
Kwa
upande wake afisa mifugo wilaya ya Karagwe Matisera Byenobi amesema kuwa kila
kata na kijiji wanatakiwa kutenga maeneo kwa ajili ya kufugia na kubaini
wafugaji waliopo na mifugo walioyonayo nah ii ni kutokana na kuwa mifugo nayo
inachangia katika uhabifu wa mazingira.
Post a Comment