Maafisa watendaji wa kata na vijiji na wenyeviti wa
vijiji na vitongoji katika kata zilizopo katika ukanda wa Bushangaro wilayani
Karagwe mkoani Kagera wametakiwa kufuatilia na kupiga marufuku wanunuzi wa
kahawa za magendo ambao tayari wameanza kuzunguka vijijini kwa wakulima kwa
ajili ya kuwalaghai kuwauzia kahawa za magendo.
Wito huo umetolewa na mkuu wa kituo cha polisi Omukarilo
wilayani Karagwe Antony Bupamba wakati akiongea na baadhi ya viongozi wa kata
za Kibondo,Nyakabanga,na Nyakakika wilayani humu.
Bupamba amesema kuwa
tayari wanunuzi wa kahawa za magendo wameshaanza kupita kwa wakulima kwa
ajili ya kununua kahawa mbichi jambo
ambalo ni kinyume na sheria ambapo amesema kuwa ni jukumu la viongozi wa vijiji
kuhakikisha wanapambana na watu wanaofanya hivyo kwa kuwafikisha katika vyombo
vya sheria.
Amesema kuwa watakaemkamata wamfikishe katika kituo cha
polisi na hatua dhidi yake sitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kulala ndani kwa
muda wa masaa 24 ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya hivyo.
Nao wananchi waliongea na mtandao huu wamekili kuwepo kwa
vitendo vya uuzaji wa kahawa za magendo huku wakijihusisha na vitendo vya
uvunaji wa kahawa mbichi na kuanika chini jambo ambalo wamelitaja kuwa ni
kutofuata ushauari wa wataalamu ambao wanaotoa kila siku.
Hata hivyo wamewataka wananchi kuacha kuitupia lawama
serikali kwani kuzidi kushuka kwa bei ya kahawa kila mwaka ni kutokana na
uvunaji mbovu wa kahawa ambao unasababisha kahawa kutokuwa na ubora.
Post a Comment