Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: OLE WAO WATAKAOTUMIA FEDHA KUNYWA POMBE WATAKUMBANA NA ADHABU
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
 MRATIBU wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wilayani karagwe mkoani Kagera Edius Rwangoga amesema kuwa walengwa wa  kaya maskini wat...

 MRATIBU wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wilayani karagwe mkoani Kagera Edius Rwangoga amesema kuwa walengwa wa  kaya maskini watakao tumia fedha hizo kwa ajili ya kuoa au kuongeza mke mwingine wataondolewa katika mfuko huo.

      Hayo yalisemwa jana na mratibu wa Tasaf Rwangoga wakati akizungumza na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Rugu,Nyakasimbi Ihembe  Bisheshe na Kituntu.

     Rwangoga alisema kuwa katika dirisha la saba (7) la uhawilishaji fedha linaloendelea wilayani humo watabaini na kuwachukulia hatua baadhi ya walengwa wa kaya maskini wanaotumia fedha hizo kwa ajili ya kuoa na kuongeza wake wengine ikiwemo pia ulevi wa kupindukia kinyume cha malengo wa mpango huo.

     Alisema kuwa kuna baadhi ya walengwa ambao wamegeuza mpango wa Tasaf kama chombo cha starehe na kusahau kuwa malengo ya mpango huo ni kunusuru kaya maskini,kuboresha Lishe,Elimu na Afya.

     Rwangoga alisema kuwa Tasaf imeweka mkakati mwingine utakao wezesha walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini kuongeza kipato kwa kushiriki katika kazi za mikono hususani katika kipindi cha hari kwa kuibua miradi yenye manufaa kwa jamii ikiwemo hifadhi ya mazingira,umwagiliaji na barabara.

     Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Rulalo kata ya Chonyonyo John Bitakwate alisema kuwa utekelezaji wa mpango huo umeongeza idadi ya wanafunzi wanao hudhuria masomo hususani katika shule za msingi kwenye maeneo ya walengwa wa mpango huo.

      Alisema kabla ya mpango huo maudhurio katika shule yake yalikuwa ni asilimia 35 na kuwa kwa sasa mahudhurio na taaluma imepanda kwa asilimia 85 kutokana na wanafunzi kuwa na vitendea kazi na sare za shule.

     Kwa upande wake Frank Gimali mhudumu wa afya kituo cha chochonyo kata ya chochonyo alisema moja ya mashariti yaliyomo kwenye mpango huo ni kahakikisha kuwa watoto wanahudhuria masomo na kupata huduma za matibabu kwenye zahanati au vituo vya afya vilivyopo kwenye maeneo yao .

     “Tumeshuhudua mahudhurio ya akina mama wajawazito na watoto kwenye vituo vya afya na hospitali kwenye maeneo ya walengwa yameongeza pia”Alisema Gimali.

       Hata hivyo amewataka waratibu wa Tasaf na wawezeshaji ngazi ya rika kutoa elimu mara kwa mara kwa walengwa wa mfuko huo ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha za Tasaf yanayofanywa na baadhi ya walengwa wa kaya maskini.
Top of Form

Bottom of Form
Top of Form
   
Bottom of Form
Top of Form

Bottom of Form

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top