Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WATUMISHI WA MAHAKAMA WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO WATAKIWA KUTOPOKEA RUSHWA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
WATUMISHI wa idara ya mahakama wilayani karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuepuka vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa wananchi wenye ma...

WATUMISHI wa idara ya mahakama wilayani karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuepuka vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa wananchi wenye malalamiko yao ili kujenga imani ya chombo hicho kwa jamii.



        Hayo yalibainishwa jana  na mtendaji wa mahakama kuu  kanda ya Bukoba Ignosia Kabale katika semina ya mpango mkakati wa mahakama ya Tanzania wa miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2020 unao lenga kufikia malengo kwa watu wote, utawala bora, kurejesha imani ya mahakama  kwa jamii pamoja na ushirikishwaji wa wadau katika kazi za mahakama iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama hiyo.

          Kwa mjibu wa mtendaji huyo aliye wakutanisha watumishi wa mahakama hiyo alisema kuwa katika kuhakikisha mpango huo unatimizwa ni vyema watumishi wa idara ya mahakama wilayani karagwe kuhakikisha wanaepuka vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa wanachi wenye malalamiko Yao kwani siyo maadili kwa watumishi wa mahakama.

      Alisema kuwa tatizo la rushwa limekuwa changamoto kubwa ya kushughulikia matatizo ya wananchi na kufanya chombo hicho kukosa imani kwa  jamii suala ambalo haliwezi kujenga heshima kwa watumishi.

     Naye mhasibu mkuu wa mahakama ya Tanzania Fanuel Tiibuza alisema kuwa suala la kutoa lugha chafu kwa wateja wa mahakama imepelekea baadhi ya malalamiko kutoshughulikiwa kwa wakati muafaka hususani katika maeneo ya vijijini ambapo baadhi ya wanachi hawajui haki zao zinazo paswa kutolewa na mahakama.

        “Utakuta mwananchi ana malalamiko yake anakalishwa kwa muda mrefu na karani bila kushughulikiwa wakati mwingine hutolewa lugha chafu pasipo kumuhudumia shida yake na kumpiga tareha “Alisema Tiibuza.

         Aidha katika kuhakikisha mpango mkakati huo unatimizwa Naibu Msajili mahakama kuu ya kanda ya Bukoba Seif Kulita alikabidhi vitabu 10 vya mwongozo wa ukaguzi wa mahakama namba za simu nchini kote Tanzania bara ofisi za mikoa na wilaya na mahakama zote,mabango kwa ajili ya elimu na utoaji taarifa,malalamiko,maoni,ushauri au pongezi kwa mahakama hiyo.




         Hata hivyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Paul Magoryo alishukuru kwa semina hiyo na kuwataka watumishi wa idara ya mahakama kuhakikisha wanayafanyia kazi maagizo hayo ikiwa ni pamoja na kutenda kazi kwa weledi wa utumishi wa umma.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top