Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: UBALOZI WA CHINA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI WA CHINA NAO WALIGUSWA NA TETEMEKO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
UBALOZI wa China, Makampuni  pamoja na Wananchi wa nchi hiyo wametoa msaada  wa vitu mbalimbali Vyenye thamani ya  shilingi milio...




UBALOZI wa China, Makampuni  pamoja na Wananchi wa nchi hiyo wametoa msaada  wa vitu mbalimbali Vyenye thamani ya  shilingi milioni 100 wa ajiri ya waathirika  waliopatwa na tetemeko la  ardhi  ili kuwasaidia katika makazi yao.

Akikabizi  misaada hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali  Mstaafu SALUMU KIJUU  , Naibu Balozi wa nchi ya China ZHANG BIAO  amesema  Baloz wa wa nchi hiyo DK Lu Youqing alizungumza na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DK John Magufuli  na kusikitishwa na tukio hilo.

BIAO  amesema  kuwa,ubalozi kwa kuunganisha nguvu za pamoja na wananchi wa nchi hiyo na kuitisha mkutano wenye kukusanya mfuko kwa waathirika wa tetemeko  kwa kununua vifaa ambavyo vitawasaidia kama , mahema,madawa chakula , maji na blanketi.


Amebainisha  kuwa, kampuni  ya ujenzi  ya kichina iliyoko nchini china imetoa mifuko ya saruji tani 80ikiwa China na Tanzania zimefanya ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kuijenga taifa katika karne iliyopita.

Kwa upande wake  mkuu wa mkoa wa KAGERA  Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU , amesema   misaada hiyo aliyoipokea atahakikisha inawafikia walengwa wote bila kujali  itikadi za  kikabila, siasa, wala dini kwa  taratibu aklizozipanga ili kufakisha zoezi hilo.

Aidha amesema tayari misaada inaendelea kutolewa kutoka kwa wananchi mbalimbali wenye kuguswa na tatizo hilo na tayari milioni 460 zimeingizwa katika akaunti ya kamati ya maafa ya  mkoa Benki iliyopo CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti Namba. 0152225617300. kwajili ya uchangiaji huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top