Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KAYA 200 ZAAMULIWA KUONDOA MAZAO YAO NDANI YA WIKI MBILI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Kaya 200 zilizolima katika vyanzo vya maji katika kijiji cha Mikale na Kiwela katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba mkoani Kagera zime...

Kaya 200 zilizolima katika vyanzo vya maji katika kijiji cha Mikale na Kiwela katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba mkoani Kagera zimepewa wiki mbili kuondoa mazao yao katika vyanzo hivyo.

Afisa kilimo wa vijiji hivyo viwili  Benedicto Karoli amesema kuwa wameshafanya utafiti katika vijiji hivyo na kubaini kuwa kuna kaya mia 2 ambazo zimelima katika vyanzo vya maji.
 Karoli amesema kuwa wananchi hao wanatakiwa kuacha tabia ya kulima katika vyanzo vya maji kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria ambapo wananchi wanatakiwa kukaa mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji ili kusaidia kutunza mazingira.

Amesema kuwa kila mwananchi anatakiwa kutunza mazingira yanayomzunguka kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kutunza vyanzo vya maji katika vijiji hivyo.
Aidha amesema kuwa kwa watakaoshindwa kutoa mazao yao katika vyanzo vya maji ndani ya wiki mbili hizo zilizotolewa watafikishwa katika vyombo vya sheria.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top