Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WANAFUNZI WAPEWA KINGA YA KICHOCHO NA MINYOO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Jumla ya wanafunzi 1057 wa shule ya msingi Kayanga Wilayani Karagwe wamepata dawa ya kinga na tiba ya kichocho na minyoo. Akizungu...

Jumla ya wanafunzi 1057 wa shule ya msingi Kayanga Wilayani Karagwe wamepata dawa ya kinga na tiba ya kichocho na minyoo.


Akizungumza na chombo hiki mwalimu Mkuu wa shule hiyo Oswardi Maliseli amesema Zoezi la  utoaji wa dawa ya kinga  na Tiba ya ya kichocho na  minyoo katika shule yake limeanza mapema leo asubuhi na kuamalizika vizuri kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema kabla ya kuanza kupata dawa hiyo,wanafunzi waliokuwa na umri wa kupata dawa hiyo ,wameanza kula chakula kama maelekezo yalivyotolewa kutoka sekta ya Afya ,ambapo chakula wamekipata shuleni ,kilichochangwa na wazazi wa watoto husika.

Kwa Upande wa wanafunzi baada ya kupata dawa hizo wameeleza kumeza dawa hizo chini ya ulinzi wa walimu wao ili wasisitupe na hakuna madhara yaliyojitokeza kwao.

Wamesema ,baada ya kumeza dawa hizo walimu waliwaonyesha sehemu ya kupumzika na kuwataka wasicheze mapaka dawa itulie ndani ili kuepuka baadhi ya watu wenye kichefuchefu kutapika.


Aidha baadhi ya wazazi walioongea na kituo hiki ,wamesema serikali imefanya vizuri kuwapatia dawa watoto wao,kwani  ni njia bora ya kulinda afya zao na kusema kuwa swala hili linawapa imani ya  kuwa na kizazi kisichoshambuliwa na magonjwa kulinda ili kuendeleza jamii iliyosafi na salama.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top