Unknown Unknown Author
Title: WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIMU NA VIONGOZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wazazi na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuunga mkoano utoaji wa dawa za minyoo na kichocho kwa watoto wao ii kuhakikisha  kutimiza waj...

Wazazi na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuunga mkoano utoaji wa dawa za minyoo na kichocho kwa watoto wao ii kuhakikisha  kutimiza wajibu wao ili kufanikisha adhima ya serikali kwa kukabiliana na magonjwa hayo.


Kauli hiyo imetolewa na Kaimu afisa Afya manispaa ya Bukoba GEREVASE ISHENGOMA wakati akizungumzia juu ya utoaji dawa unaoendelea shuleni kwa watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 14.

Amesema kuwa magonjwa ya Minyoo ya Tumbo mkoani Kagera bado yako juu ambapo utafiti uliofanyika mwaka 2016 katika baadhi ya shule za msingi Halmashauri nne  shule iliyoongoza ni kasosibakaya iliyoko halmashauri ya Bihalamulo kwa asilimia 84 ikifuatiwa na shule ya msingi Ibuga iliyoko Ngara kwa asilimia 71.


Hata  hivyo ISHENGOMA amesisitiza kuwa kabla ya watoto kupewa dawa watoto wanapaswa wawe wamekula kabla ya masaa mawili pamoja na kushiba vizuri ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top