Unknown Unknown Author
Title: WANYEVITI WA VIJIJI MULEBA WAMETAKIWA KUUNDA KAMATI ZA KULEVYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wenyeviti wa vijiji na watendaji wa ngazi zote   katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba wameagizwa kuunda kamati ya kudhibiti madawa ya...

Wenyeviti wa vijiji na watendaji wa ngazi zote  katika kata ya Kabilizi wilayani Muleba wameagizwa kuunda kamati ya kudhibiti madawa ya kulevya katika kata hiyo .

Agizo hilo limetolewa na diwani wa kata ya Kabilizi Solomoni Karuga wakati akikagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na wakazi wa kata hiyo.


 Karugaba amesema kuwa viongozi hao wanatakiwa kuunda kamati ambayo itazungukia maeneo yote ya kata hiyo kutoa elimu juu ya madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya . na kuhakikisha hakuna matumizi ya aina yoyote ya madawa ya kulevya wala kijiji kinachojishughulisha na ulimaji wa bangi katika maeneo yao.


Karugaba amesema kuwa kamati hiyo itakayoundwa inatakiwa kuwa inatoa taarifa kwa kila eneo itakalokuwa inazungukia  jambo ambalo litasaidia kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya kwani vita hiyo ni yakila mmoja .


Hata hivyo ameongeza kuwa baada ya kubaini  kuwa vitendo hiyo kuwa vipo kwenye  kata  hiyo wanatakiwa kutoa taarifa kwa diwani huyo mara moja ili hatua za kisheria zifuatwe.
Aidha amesema kuwa kata hiyo yenye vijiji vitano bado haijabaini kuwepo kwa matumizi ya madawa ya kulevya au kuwepo kwa eneo linalolima bangi mpaka sasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top