Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MGOGORO WA ARDHI MISSENYI WAENDELEA KUWATESA WANANCHI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wakazi wa vitongoji sita kati ya tisa vilivyoko katika kijiji cha Bubale kata Kakunyu wilayani Missenyi, wameomba serikali kusaidia kuta...

Wakazi wa vitongoji sita kati ya tisa vilivyoko katika kijiji cha Bubale kata Kakunyu wilayani Missenyi, wameomba serikali kusaidia kutatua mgogoro wa ardhi unaowakabili, ambao umesababisha kuishi maisha magumu kwa kukosa chakula na makazi.

Wakizungumzia hali hiyo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Nkenge dokta Diodorus Kamara, wananchi hao wamesema kuwa, ugumu huo wa maisha umeotokana na makazi yao kuteketezwa kwa moto na kufukuzwa katika mashamba yao, wakidaiwa kuishi ndani ya vitalu vya wawekezaji.

Wananchi hao akiwemo Msafiri Sevelin na Rebeca Mussa wamesema kuwa, mazao yao yaliyoko katika mashamba waliyolima kwa nguvu zao, kwa sasa yanatumika kulishia mifugo, huku wakidai kuwa baadhi yao wanalala nje kutoka na nyumba zao kuchomwa moto.



Akizungumza na wananchi hao mbunge wa jimbo la Nkenge dokta Kamala amesema kuwa,  ipo tume ambayo iliundwa  na waziri mkuu ili kufuatilia mgogoro huo wa wakulima pamoja na wawekezaji katika lanchi ya Missenyi, na kueleza kuwa hatakubaliana na tume hiyo iwapo ripoti yao haitazingatia mahitaji ya wananchi.



Mgogoro huo kati ya wananchi na wawekezaji katika vitalu hivyo umeanza karibia miaka kumi na moja iliyopita, hadi sasa bado ufumbuzi haujapatikana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top