Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MAJENGO NA MIUNDO MBINU YA CHUO KIKUU KARAGWE (KARUCO)
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Miundo mbinu na majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Karagwe (KARUCO), Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kinachomilikiwa na  Kanisa la K...



Miundo mbinu na majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Karagwe (KARUCO), Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kinachomilikiwa na  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya  Karagwe,  inayotajwa kujengwa kwa takribani shilingi bilioni mbili na nusu imezinduliwa  Jumapili ya tarehe 29 Oktoba, 2017 katika sherehe zilizoenda sambamba na maadhimisho ya Jubilei ya miaka 500 ya Matengenezo ya kanisa hilo.


KARUCO kilichojengwa kwenye eneo la Kishoju, Kata ya Kihanga kikiwa na takribani  eneo la ekari zipatazo 912.2 kinatarajiwa kufundisha program za  kilimo na stadi za mazingira pindi kitakapo pata Ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) huku kikielezwa kuwa kukamilika kwake kunakifanya kuwa  chuo kikuu cha pili ukiacha kile cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ambacho ndio pekee kinachofundisha  stadi hizo za kilimo hapa nchini.


Ujenzi wa Miundo mbinu na majengo ya chuo kikuu hicho ulizinduliwa mnamo Oktoba 11, 2012 na aliyekuwa waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika kwa  wakati huo, Mhandisi Chrisopher Chiza.




Sherehe hizi za uzinduzi zilizofanyikia katika viwanja vya chuo kikuu hicho, ambapo zilianza na ibada ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa, adhimisho linalotajwa kuwa ni kumbukumbu  muhimu ya miaka hiyo tangu kanisa hilo lilipoasisiwa duniani na Mkuu wa kanisa hilo, mchungaji Dkt. Martine Luther.


Baada ya kumalizika kwa sehemu ya kwanza ambayo ni Ibada iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Mhashamu Dkt. Benson Bagonza, uzinduzi wa majengo na miundombinu ya chuo kikuu hicho ulifanyika.


Sherehe hizo zilizowakusanya mamia ya watu kutoka ndani na nje ya Wilaya ya Karagwe zilihudhuliwa na viongozi kadhaa wa serikali, viongozi wa dini na wafadhili mbalimbali toka nje ya nchi ambao kwa kiasi kikubwa wamefadhili ujenzi wa chuo kikuu hicho.


Viongozi wa serikali waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mh. Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Mustapha Kijuu ambaye kipekee alimwakilisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  aliyetajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho haya lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake hakuweza kuhudhuria na kumuomba Mkuu wa Mkoa huyo kumwakilisha.


Mkuu wa Mkoa  aliambatana na viongozi  wote wa kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Mh. Diwani Athumani.




Pia alikuwepo Mkuu wa Wilaya Karagwe, Mh.Godfrey Mheluka, wajumbe  wa kamati ya usalama ya wilaya, Mkuu wa Wilaya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro, Mkuu wa Wilaya Kyerwa, Mh. Kanali (Mst.) Shabaan Lissu pamoja na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Karagwe pindi ujenzi wa miundo mbinu hiyo ulipozinduliwa, Mh. Darry Rwegasira ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya mstaafu.


Wengine walikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, Mh. Wallace Mashanda pamoja na baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya hii huku Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya, ndugu Ashura Kajuna na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri wakishiriki pia.


Sherehe hizi zilihudhuriwa pia na viongozi wa dini toka madhehebu mbalimbali ya ndani na nje ya nchi na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa.
Awali Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Profesa Joseph Parsalaw, alimpongeza Askofu Dkt. Bagonza kwa juhudi kubwa zilizofanyika katika ujenzi huo huku alitanabaisha kwamba alikuwepo kwenye eneo hilo wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo.
Huku akibainisha kwamba ukamilishwaji wa ujenzi wa KARUCO unakifanya chuo kikuu cha Tumaini Makumira kufikisha idadi ya vyuo vikuu vishiriki vitano.


“Naamini hata wachungaji waliokuwepo kwenye eneo hili wakati ule ujenzi wa miundombinu hii ulipozinduliwa walikuwa hawana matumaini ya kufikia hatua hii iliyofikiwa leo lakini kwa sisi tunaomfahamu askofu Dkt. Bagonza tuliamini tutafika hapa tulipofika”, alisema Prof. Parsalaw.




Mapema Askofu, Dkt. Bagonza, wakati alipokuwa akimkaribisha Mgeni rasmi alielezea furaha yake katika kuona juu ya kukamilika kwa ujenzi wa  miundo mbinu na majengo huku akiahidi kukamilika kwa ujenzi wa baadhi ya miundombinu ambayo haijakamilika ili kuwapa nafasi  Tume ya Vyuo Vikuu kufanya ukaguzi kwa ajili ya kutoa ithibati na masomo yaweze kuanza kwa mwaka 2018/2019 kama ilivyokusudiwa.


“Hadi sasa tayari miundombinu ya maji imekamilika kwa sehemu kubwa, Bweni la kulala wanafunzi wa kike limekamilika, jengo la utawala limekamilika, maabara zote zinazohitajika zimekamilika pamoja na Maktaba”, alisema askofu Dkt. Bagonza.


“Miundo mbinu nyingine pia imekamilika  ikiwemo madarasa  na samani mbalimbali zitakazotumiwa na wanafunzi zimewekwa’’, alisema


Akifafanua juu ya program zitakazo fundishwa chuoni hapo, Askofu Dkt.  Bagonza alibainisha kuwa wataanza na progranu za Kilimo, Mifugo, Misitu, Mazingira, Nyuki na Teknolojia ya Habari.


Aidha, Askofu Dkt. Bagonza amezitaja baadhi ya fursa ambazo wananchi wa Karagwe  watanufaika nazo ikiwemo kupanua soko la mazao yao na mifugo  na kuikuza Wilaya kiuchumi  baada ya kuwa na wataalam karibu ambao pia watasaidia katika kuongeza thamani katika mazao ya wakulima na kutafuta soko la pamoja.



Faida nyingine ni kwamba uwepo wa chuo kikuu pia utasaidia kupeleka maendeleo vijijini, kuwa chemchem ya ajira, utafiti, uwekezaji, kuchochea mabadiliko katika sekta za afya, huduma nyingine kama kituo cha polisi, mawasiliano n.k


Katika hatua nyingine, Askofu Bagonza ameeleza kufurahishwa na  ushirikiano anaopata kutoka kwa viongozi wa wilaya tangu miaka ya  1980 hadi sasa ambapo wanaenda kushuhudia hatua kubwa sana  ya maendeleo Karagwe.


Kuhusu umiliki wa chuo, imefafanuliwa kuwa chuo hicho ni mali ya wananchi wa Karagwe bila kujali tofauti zao za kiimani na kwamba kinaendelea kuchangiwa na watu mbalimbali kwani kinalenga kwenye mapinduzi ya kiuchumi na kijamii Wilayani Karagwe.


’Licha ya chuo hiki kusajiliwa kwa jina la Kanisa lakini ni mali ya wananchi wote wa Karagwe na kinaendelea  kuchangiwana waumini wa dini zote  hivyo natoa wito kwa kila mmoja wetu kuunga mkono jitihada hizi ili kuinua maendeleo ya wilaya yetu na taifa kwa ujumla.’’ alisema Askofu Bagonza


Ili kuwezesha wakulima kupata soko nzuri la mazao yao, Askofu Dkt  Bagonza amebainisha kuwa  mara baada ya chuo kuzinduliwa, upo mpango wa kujenga  vituo vya fursa vitano( Opportunity Centers )  ambapo vituo hivyo vitakuwa na miundombinu ya kila aina ikiwemo ya kuhifadhi mazao yasiharibike  na kwamba wakulima watakuwa wanauzia mazo yao katika vituo hivyo kwa umoja ili wawe na sauti ya pamoja ya kupanga bei ya mazao tofauti na ilivyo hivi sasa.


Mgeni rasmi, Rais wa Mstaafu wa Awamu Nne, Mh.Dkt. Jakaya Kikwete katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa huu ameahidi kushirikiana na KARUCO kupitia Taasisi yake ya Jakaya Kikwete katika shughuli za kilimo.


“Kiu yangu ni kuona wakulima wadogo wanaongeza tija katika Kilimo”, alisema Dkt. Kikwete kupitia hotuba hiyo.


Katika hatua nyingine askofu Dkt. Bagonza alimwombea heri Rais mstaafu Kikwete ili aweze kufika pindi chuo hicho kitakapozinduliwa baada ya kupata ithibati na TCU) ya kunza kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kama ilivyokusudiwa nah ii ni kutokana

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top