Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MBUNGE WA JIMBO LA KARAGWE AMUANGUKIA DK JAKAYA KIKWETE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Mbunge wa jimbo la Karagwe, Mh. Innocent  L.  Bashungwa  amemwomba Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh, John Pombe Maguful...






Mbunge wa jimbo la Karagwe, Mh. Innocent  L.  Bashungwa  amemwomba Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh, John Pombe Magufuli  kusaidia  katika kukamilisha mradi wa maji wa Rwakajunju  ili kuwatua ndoo kichwani wananchi wa Karagwe hususani akina mama.


Maombi hayo kwa Rais yametumwa kupitia  aliyekuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa majengo na miundombinu ya kinachotarajiwa kuwa chuo kikuu cha Karagwe ( KARUCO)  Mh, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambaye naye pia aliwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Mh, Meja Jenerali ( Mst) Mustafa  S.Kijuu baada ya Mh, Kikwete kushindwa kufika kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezowake.

Mradi huu wa maji ulianza kupangwa tangu kipindi cha awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete lakini hadi sasa haujawahi kukamilika, Mh Rais Mstaafu, nakuomba ufikishe kilio hiki kwa Rais Magufuli ili mradi huu uweze kuanza kwani shida ya maji kwa Karagwe nikubwa mno, naongea hivi nikiwa nimepiga magoti kama ishara ya kuonesha ukubwa wa tatizo hili”, alisema Mh. Bashungwa.



Kwa vipindi tofauti, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana na kuwafikia wananchi  kwa urahisi, ufanisi na kukidhi mahitaji.
Pamoja na jitihada hizo , huduma ya maji kwa mji wa Kayanga  na baadhi ya vijiji Wilayani Karagwe imekuwa ya kiwango cha kutoridhisha kutokana na halihalisi ya jiografia ya eneo lenyewe kwani vyanzo vya maji  vilivyopo katika baadhi ya maeneo  havina maji ya kutosha .


Licha  ya vyanzo vingi vya maji kutokuwa na maji ya kutosha, vyanzo hivyo vinapatikana katika maeneo ya mabondeni  huku makazi ya watu yakiwa maeneo ya juu kwenye miinuko  na hivyo kuhitaji  gharama kubwa za ujenzi wa miradi ya maji na uendeshaji wake.


Kutokana na hali hiyo, Serikali ilishaweka katika mipango yake  Mpango wa usanifu  na hatimaye ujenzi wa mradi wa maji kwa manufaa ya wakazi  wa makao makuu ya mji wa Wilaya  na vijiji vyote  jirani .


Hata hivyo, kuna vijiji 30 vilivyopendekezwa kunufaika na mradi huu wa maji kutoka ziwa Rwakajunju ambapo vijiji hiyo ni Ahakishaka, Kashanda , Ndama, Nyabiyonza, Nyamieri, Nyabwegira, Chabalisa , Nyakagoyagoye, Kagutu, Kafuro, RularoKishoju na Nyakaiga.


Vijiji vingine ni Kiruruma, eneo linalotajiwa kuwa chuo Kikuu cha Karagwe – KARUCO University, Kakuraijo, Kamagambo, Mlamba, Omukakoto, Chonyonyo, Nyamizi, Nyakashenyi, Omukimeya, Katembe, Nyakisheshe, Ihanda, Bisheshe  Omurusimbi, Rukole na Kituntu.


Hadi sasa kazi inayotarajiwa kukamilika ni kukamilisha upembuzi yakinifu  na kuingiza vijiji vyote kwenye mwambao wa mradi.

Kwa mujibu wa ‘BUWASA’ ambao wanasimamia zoezi hili kwa niaba ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wamesema kwamba wanatarajia  kuwa taratibu za kumpata mshauri elekezi utakuwa umekemilika mapema  mwishoni mwa mwezi Januari  2018 .
Miongoni mwa kazi za mshauri elekezi itakuwa ni pamoja na kukamilisha ‘design’ na kuandaa makabrasha ya zabuni .


Mradi wa maji kutoka ziwa Rwakajunju unakadiriwa kugharimu dola za kimarekeni millioni 70.7  ambapo kilio cha mbunge wa jimbo la Karagwe ni kuona serikali inatoa fedha hizo kwa wakati ili mradi uanze kwani changamoto ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Karagwe nikubwa sana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top