Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa
na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini Dar es
salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais, Dkt. John
Magufuli alikua mgeni rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
Wimbo wa Taifa
ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria
Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa
ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji
Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam, Said Mecki Sadiki.
Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya ulinzi
na usalama nchini na wadau muhimu wa Mahakama waliohudhuria Maadhimisho
ya Siku ya Sheria wakitoa heshima zao wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS), Charles Rwechungura akitoa salam na ujumbe wa Chama hicho wakati
wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue (kulia) akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi
mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia kwake ni
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga.
Jaji Mkuu wa Mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohamed Chande Othman akiwahutubia viongozi, mabalozi na wageni
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku
ya Sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu utendaji wa
Mahakama na Utoaji wa Haki kwa wananchi kwa wakati kwenye maadhimisho ya
Siku ya Sheria. Mhe. Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo
yaliyohudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya
nchi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na Majaji wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa kilele cha Siku
ya Sheria nchini.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa dini na baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na
Usalama na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wakati wa kilele
cha Siku ya Sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili.
Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga
(kulia) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu kutoka nchini Kenya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar
es salaam. Jaji Mkuu wa Kenya alikua miongoni mwa wageni mashuhuri
walioalikwa na Mahakama ya Tanzania kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya
Sheria.
Wageni mbalimbali waliohudhuria
maadhimisho ya Siku ya Sheria wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli aliyokua akiitoa leo jijini
Dar es salaam.
Post a Comment