Jumla ya watumishi 10 hewa
wamebainiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja
kwenye idara ya elimu na afya katika halmashauri ya wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera.
Taarifa hiyo imetolewa na
mkuu wa idara ya utawala na utumishi wa wilaya hiyo Nikolaus Massawe katika
baraza la madiwani lililofanyika kwa siku
mbili April 28 na 29 mwaka huu.
Massawe amesema watumishi
hao wamebainika kwenye idara ya elimu ya sekondari na msingi pamoja na idara ya
Afya ambao tayari majina yao
yameishawasilishwa katika ofsi ya Katibu Tawala mkoa wa Kagera ili sheria ichukue mkondo wake .
Hata hivyo afisa utumishi huyo
amesema kuwa bado wanaendelea na zoezi
la kufanya uhakiki wa watumishi wote kwa kila idara ili kuwabaini watumishi
wengine hewa zaidi kama wapo.
Post a Comment