Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya
Karagwe kimewavua rasmi uanachama Jeni
Pesha,Idda Bangatwire na Deusdeth Kahangwa kwa tuhuma za kutokana
kukihujumu chama hicho wakati wa uchaguzi
mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Karagwe Gregory Gabone ambaye
pia ni mwenyekiti
wa mkoa wa chama
hicho.
Gabone amesema kuwa Chama cha Demokrasia na maendeleo
Chadema Wilaya ya Karagwe baada ya
kuchunguza na kujiridhisha waliofukuzwa uanachama walishiriki kukihujumu chama wakati wa uchaguzi mkuu
uliofanyika oktaba 25 mwaka jana uongozi wa
chama umeona kiwavua uanachama
huo ili kuwaruhusu
kuendelea na shughuli
zao nyingine nje
ya chama.
Gabone amesema wahusika hao walovuliwa uanachama wa
Chadema kuanzia sasa chama hakiwatambui na amewaomba wananchi na viongozi kwa
ujumla kutowapa ushirikiano wowote unaohusiana na shughuli zozote za chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA)
Post a Comment