Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) YATOA TAMKO KUHUSU BUNGE.
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Siku moja baada ya kuibuka vurugu Bungeni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) leo kimetoa tamko lenye maagizo matano iki...




Siku moja baada ya kuibuka vurugu Bungeni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) leo kimetoa tamko lenye maagizo matano ikiwamo wabunge wote waliosimamishwa kurejeshwa bungeni ili kuendelea na majukumu yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Dk Helen Kijo Bisimba alitaja maagizo mengine ni kuitaka serikali isitishe uamuzi wake wa kuwafukuza wanafunzi wa UDOM na badala yake itafutwe suluhu kwa amani.

"Tatu, tunalitaka bunge kutimiza wajibu wake kikatiba kuishauri,kuisimamia na kuiwajibisha serikali inapokosea,"alisema.

Bisimba alisema pia Naibu spika na mwenyekiti wa bunge kufanya uamuzi bila upendeleo na wazingatie maslahi ya watanzania.

Katika tamko hilo alimaliza kwa kuwataka watanzania wote wasimamie kidete kuhakikisha wabunge wao wanaendelea na kazi waliyowatuma.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top