Watu wawili
wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti baada ya kujinyonga katika kata
ya Nyanga na Buhembe manispaa ya Bukoba.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera AUGUSTINE OLLOMI amesema kuwa katika tukio la
kwanza mtu mmoja aitwaye RAPHAEL IGNAS mwenye umri wa miaka 72 amekutwa kwenye
shamba la jirani yake akiwa amejingonya na kamba ya mgomba kwenye mti wa
muembe.
Kamanda OLLOMI amesema kuwa,tukio la pili ni lile lililomhusisha RESPICIUS
ELIMANI mwenye umri wa miaka 45 ambaye amekutwa amejingonga nyumbani
kwake kwa kutumia kamba ya manira kwenye mti wa Mparachichi.
Aidha ameongeza kuwa mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na jeshi hilo na
chanzo cha vifo hivyo hakijajulikana hivyo polisi inaendelea na uchunguzi.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment