·
Bodi na Meneja Mkuu wa KCU 1990 LTD
Wasimamishwa Kazi Kuanzia Sasa
·
Nafasi ya Mrajisi Msaidizi Kagera
yasitishwa na Kuteuliwa Mwingine.
·
Akaunti zote za KCU 1990 LTD Zasitishwa Kupisha
Uchunguzi
Bodi ya Chama Kikuu cha
Ushirika Mkoani Kagera, Kagera Co operative Union 1990 LTD (KCU)
pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho na
Mrajisi Masidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera wamesimamishwa kazi
kuanzia leo tarehe 21.07.2016 kwa tuhuma za ubadhilifu zaidi ya shilingi
milioni 900 pamoja na kuingia mikataba yenye harufu ya rushwa iliyopelekea
hasara kubwa kwa Chama hicho Kikuu cha Ushirika
Mkoani Kagera.
Kaimu Mrajisi wa Vyama vya
Ushirika Nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akitangza rasmi kusimamishwa kwa
Bodi ya KCU pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho cha Ushirika alisema kuwa Bodi
hiyo ikishirikiana na Meneja Mkuu Bw. Vedastus Ngaiza walitoa taarifa za uongo
katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho wa mwezi Mei 2016 kuhusu deni wanalodaiwa na
Benki ya CRDB.
Dkt. Rutabanzibwa alisema
baada ya kutuma wakaguzi kutoka ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini,
Wakaguzi hao walibaini kuwa taarifa waliyosomewa wananchama katika mkutano
ilitaja kuwa deni lilikuwa Shilingi bilioni 2.8 kumbe haikuwa kweli kwani deni
lilikuwa limepanda hadi shilinngi bilioni 3.15 Bodi na Meneja Mkuu walikuwa
wamewadanganya wanachama wa chama hicho.
Pili,
Wakaguzi hao waligundua kuwa shilingi Milioni
124 zilitumika katika malipo na hakukuwa na maelezo ya kutosheleza kuhusu
malipo ya fedha hizo. Tatu, KCU
iliingia mikataba ya kukodisha majengo yake
amabayo haikufuata bei ya soko
kwa sasa, na mikataba hiyo ilifungwa kwa makubaliano ya miaka 10 jambo ambalo
linapelekea Chama hicho kulipwa pango kwa bei ya chini kabisa isiyoendana na
soko.
Nne,
Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU kimekuwa kikinunua kahawa ya kiwango
cha chini kabisa na kusababisha hasara kubwa. Tano, Chama cha KCU kilijiingiza kataika miradi isiyokuwa na tija
kama mradi wa kununua maharage ambao ulikisababishia hasara kubwa Chama hicho.
Dkt. Rutabanzibwa alisema
kuwa kutokana na sheria Na. 6 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi wa Vyama vya Ushirika
nchini Bodi ya KCU hakufanya kazi yake ipasavyo ya kukisimamia vizuri chama
hicho Aidha, Bodi hiyo ilifanya vikao 12 kwa mwaka jana 2015 vikao ambavyo
vinaonekana havikuwa na tija kwani pamoja na vikao hivyo vya Bodi kufanyika
bado kulikuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha.
MAELEKEZO
Dkt. Ruatabazibwa
baada ya kutaja ubadhirifu uliofanyika katika Chama Kikuu cha Ushirika KCU
alisema kuwa Serikali imeamua kuchuka hatua zifuatazo;
1. Kufuta
Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU iliyoteuliwa mwaka 2014
2. Kusitisha
ajira ya Meneja Mkuu wa KCU Bw. Vedastus Ngaiza mpaka hapo uchunguzi wa tuhuma
za ubadhirifu wa fedha utakapokamilika.
3. Kusitisha
nafasi ya Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Bw. Nestory Shorozi kwani
ubadhirifu huo ulifanika yeye akiwepo bila kukishauri vizuri Chama hicho Kikuu cha Ushirika .
4. Akaunti
zote za Chama cha Ushirika KCU kusimamishwa mara moja mpaka hapo utaratiibu
mzuri utakapokuwa umewekwa .
KUNUSURU
CHAMA
Dkt.
Rutabanzibwa alisema kuwa katika kukinusuru Chama Kikuu cha KCU pia na
kuendelea na Msimu wa manunuzi ya kahawa Serikali imefanya uteuzi mdogo wa Mrajisi
Msaidizi Bw, Robert Makene Mtambo kutoka Ukerewe Mkoani Mwanza atakayeshikiria kwa muda nafasi ya Bw.
Nestory Shorozi aliyekuwa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera.
Aidha
mrajisi Msaidizi aliyeteuliwa Bw. Mtambo
atakaimu nafasi ya Meneja Mkuu wa KCU iliyokuwa ikishikiliwa na Bw.
Vedastus Ngaiza. Katika kukaimu nafasi hiyo Bw. Mtambo atatakiwa kuitisha
Mkutano Mkuu wa wanachama wa KCU ndani ya mwezi mmoja na katika mkutano huo atateuliwa Mwenyekiti
ambaye atatakiwa kusoma taarifa halisi ya KCU iliyotakiwa kusomwa mwezi Mei
2016 katika Mkutano Mkuu.
Adha
Dkt. Rutabanzibwa alisema Serikali haikukurupuka kuchukua hatua hiyo bali
ilifanya uchunguzi wa kutosha ikiwa ni pamoja kuipa bodi nafasi ya kujieleza
lakini haikutoa maelezo ya kutosha na badala ya kupunguza deni wao waliliongeza
deni likapanda zaidi. Pia Dkt. Rutabanzibwa aliviagiza vyombo vya uchunguzi
kama TAKUKURU, Polisi na Usalama kuanza kulifanyia kazi suala hilo mara moja.
Kaimu
Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa alimalizia kwa kusema
kuwa Serikali imeamua kulifanyia kazi suala la VyamaVikuu vya Ushirika nchini
kwani vyama hivyo vimeonekana kuwa badala ya kuwasaidia wakulima vinawadidimiza
ambapo alisema walianzia Mwanza, sasa Kagera, na wanaelekea Mikoa ya Geita,
Simiyu, na Shinyanga.
Post a Comment