Simanzi,siku
moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari
ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti
la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya
Mwangosi,SHUJAA JOSEPH SENGA,amefariki dunia usiku huu.
Senga
amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Bila
Joseph Senga,shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila woga,akapiga
picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha,huku anga ikiwa
imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,milio ya risasi ikisikika,na
kuzitunza,zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi,leo hii asingekuwa
Senga,nadhani kusingekuwa na kesi na
mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.Nakulilia Senga..
Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu
aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua,Senga umekwenda wadogo zako
katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga,Senga,kamsalimie
Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie
mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.
Nenda
Senga,picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika
mazingira hatarishi.
Post a Comment