Viongozi wa dini mkoani KAGERA wameshauriwa kuimarisha ulinzi katika
nyumba za ibada ili kuepusha vitendo vya wizi vinavyojitokeza wakati wa
ibada.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA ABEL MTAGWA ameyasema hayo
kufuatia wizi wa pikipiki yenye namba za usajili MC 347ADP aina ya SUNLAGE
inayomikiwa na BENEDICTO KAMUGISHA ilipoibiwa wakati ibada ikiendelea katika
kanisa la Kiinjili la kirutheri Bukungu kata ya Kamachumu wilayani Muleba.
Kamanda MTAGWA amesema kuwa upelelezi na uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea wa kubaini nani iliiba pikipiki hiyo.
Aidha amewataka viongozi wa makanisa kuajili walinzi wenye ueledi na kazi hiyo
ili kupunguza changamoto za wizi zinazojitokeza.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment