CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelaani vitendo vya vurugu
vinavyochochewa na viongozi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli
hiyo imetokana na kitendo kilichotokea jana katika Halmashauri ya
Kilombero kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Mbunge
wa Kilombero, Peter Lijualikali aliondolewa kwenye ukumbu wa mkutano
kwa kukokotwa na polisi baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho,
Azimina Mbilinyi kutoa amri atolewe nje.
Sababu
za kutolewa mbunge huyo zilielezwa kuwa hakupaswa kuwepo na kushiriki
upigaji kura ambapo mwenyekiti huyo alidai amepokea maelekezo hayo
kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo kwenye Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es
Salaam, Kaimu Katibu Mkuu chama hicho, Salim Mwalimu amesema, kitendo
alichofanyiwa Lijualikalini ni cha uzalilishaji.
“Naamini
kwamba matukio yanayofanywa katika halmashauri ambazo Ukawa tumeshinda
yanapangwa na CCM kwa kushirikiana na serikali yake.
“Kwanini matukio ya uzalilishaji yafanyike kwenye maeneo ambayo sisi tumeshinda na si maeneo ambayo wao wameshinda?” amehoji Mwalim.
Mwalim
amesema, Halmashauri ya Kilombero inaongozwa na Ukawa kutoka na kuwa na
madiwani na wabunge wengi kuliko CCM na kwamba uchaguzi huo
umeghairishwa kwa mara ya tatu. CCM wana madiwani pamoja na wabunge viti
maalumu 18 huku Ukawa wakiwa na 20.
“Pamoja
na ushindi wa Ukawa kuonekana waziwazi lakini bado CCM wanaleta
filigisufiligisu ya kuleta hata wabunge wa nje ilimradi tu washinde.
“Hawataweza
kutushinda hata kwanini maana hata sisi tukipeleka wabunge toka nje
bado tutawapita. Na hiyo ni ishara ya kutuogopa,” amesema Mwalimu.
Hata
hivyo, Mwalim amesema kutokana na kitendo alichofanyiwa mbunge huyo
jana wanaitaka serikali kulichukulia uzito suala hilo na kuhakikisha
mkurugenzi huyo aliyetoa amri kwa polisi kutumia mabavu kumtoa nje
mbunge huyo achukuliwe hatua za kinidhamu.
Pia,
wamemtaka mkurugenzi huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho
kuonesha barua aliyotumiwa na Simbachawene ya kutoa amri ya kumtoa nje
mbunge huyo.
Mbali
na hilo, pia ametoa rai kwa serikali kufuata misingi bora ya uongozi
haswa katika kusimamia masuala ya nayowahusu wananchi hususani suala la
Meya wa Jiji ambalo bado halijafanyika.
Post a Comment