MBUNGE
wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ),
Freeman Mbowe ameibana serikali leo na kutaka ieleze ni kwanini askari
wa jeshi kutoka bara wanapelekwa Zanzibar kwa ajili ya kupiga kura
wakati wa kipindi cha uchaguzi jambo ambalo linaweza kuzua vurugu.
Mbowe
alitoa kauli hiyo bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa
kutaka kujua ni lini serikali itaacha kufanya mchezo huo ambao unaweza
kusababisha vurugu.
Pia
Mbowe alitaka kujua kama serikali inatambua kuwepo kwa vitendo hivyo
vya askari kutumika kutoka Bara na kama inajua jambo hilo na ni hatua
gani zinafanyika ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinavyoweza
kusababisha kuwepo kwa vurugu za kisiasa.
Awali
katika swali la msingi la mbunge wa Shaurimoyo Mattar Ali Salum (CCM)
alitaka kujua serikali ina mapango gani madhubuti wa utoaji ajira kwa
upande wa Tanzania Zanzibar.
Katika
swali hilo la msingi pia Salum, alitaka kujua ni asilimia ngapi ya
vijana wanaoajiriwa kutoka upande wa Zanzibar na ni kwanini utoaji wa
ajira katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa upande wa
Zanzibar usijielekeze kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU)
tu.
Akijibu
maswali hayo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein
Mwinyi akianza na swali la nyongeza la Mbowe amesema, majeshi yote ni
vyombo vya Muungano .
Akizungumzia
kupiga kura amesema utaratibu wa kupiga kura unafahamika na hivyo siyo
rahisi askari wanaokwenda Zanzibar wanaweza kupiga kura bila kufuata
utaratibu wa eneo husika.
Akijibu
swali la msingi Dk. Mwinyi amesema jeshi la wananchi wa Tanzania lina
utaratibu wa kuandikisha askari wake wapya kupitia makambi ya Jeshi la
Kujenga Taifa.
Amesema
Jeshi la Ulinzi la Wananchi halina wa Tanzania halina utaratibu wa
kuandikisha vijana kwa kufuata asilimia bali ni vijana wanaokuwa na sifa
zinazohitajika bila kujali anatoka pande gani ya Muungano.
Post a Comment