Serikali
imeliagiza jeshi la polisi na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
kuwakamata, kuwahoji na kuwafikisha mahakamani viongozi na watendaji
wote hata kama wamestaafu madaraka yao, walio husika kutoa shamba la
hekari 3,500,Morogoro.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi, baada ya kutembelea kijiji hicho cha
Mlilingwa,Ngerengere kwa lengo la kujiridhisha juu ya mwenendo mzima wa
utoaji wa eneo hilo ambao ulitiliwa mashaka na Rais.
Mhe.
Lukuvi amelazimika kukagua sahihi za wana kijiji walio orodheshwa
majina yao ambapo wengi wa waliohojiwa wamezikana sahihi hizo na kueleza
kushangazwa na hali hiyo na hata baadhi ya majina yaliyotumika sio ya
wanakijiji wenzao na kudai katika kikao hicho hakuna mwenyekiti, mjumbe
wala mtendaji aliyekuwa kwenye sakata hilo aliyehudhuria kikao hicho.
Mwakilishi
wa kampuni ya Oxfod Trading LTD aliyehudhuria mkutano huo wa kijiji,
ameonekana kushindwa kujieleza vyema pale alipokuwa akihojiwa maswali
kwa madai bado ni mgeni katika kampuni hiyo na hakuwepo wakati wa
mkutano wa kuidhinisha kutolewa kwa eneo hilo.
Baada
ya kujiridhisha, waziri Lukuvi ameagiza mtu huyo kukamatwa na ofisa wa
polisi ili kusaidia kukamatwa kwa wahusika wote wa sakata hilo na pia
kuagiza uchunguzi kufanywa kwenye ofisi zote ili watakaobainika kuhusika
na udanganyifu huo wafikishwe mahakamani
Waziri
Lukuvi amesema zoezi hilo litakuwa endelevu nchi nzima hivyo
kutahadharisha kama kuna mwekezaji yeyote aliyejipatia ardhi kwa njia ya
udanganyifu bila kufuata taratibu, ni vyema akaanza upya kufuata
maagizo ya serikali,na ikibainika kuna kosa popote shamba lake
litafutiwa milki yake na kubadilishwa matumizi kwa mujibu wa sheria.
Post a Comment