Watu
wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha mto Kilombero
kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi na
kukifanya kigonge nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo
kupinduka ndani ya maji jana usiku.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa leo Bungeni na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama, kivuko hicho kilikuwa na watu 31, magari na mizigo mbalimbali ambapo mpaka sasa mtu mmoja bado hajapatikana.

Post a Comment