Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUPORA KIASI CHA SH 15.2 MILLIONI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
MKAZI mmoja wa jijini Dar es salaam   Husein Nahim (34 )amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Karagwe MKOANI Kagera  kwa tuh...





MKAZI mmoja wa jijini Dar es salaam  Husein Nahim (34 )amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Karagwe MKOANI Kagera  kwa tuhuma ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 15 kwa mkazi wa kata ya Kihanga wilayani Karagwe.

Akisoma shitaka hilo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Paul Magoryo alisema kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa  hilo februali 25 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi wilayani humo.

Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspecta Stividana Webiro aliieleza Mahakama hiyo kwamba, mtuhumiwa siku ya tukio alipita katika eneo la kata ya Kihanga wilayani Karagwe akiwa anaendesha gari lenye namba za usajiri T 381 BWM aina ya Toyota Kalina pamoja na wenzake wawili waliokuwa ndani ya gari hilo majira ya saa mbili asubuhi  ambapo mtuhumiwa alipofika eneo hilo alisimamishwa na mlalamikaji wa kesi hiyo Godwine Kigo (22) mkazi wa kata hiyo ambaye alikuwa mkusanya ushuru na kumtaka  kumsafirisha ndani ya gari hilo hadi mjini Kayanga na wakakubaliana kuwa alipe nauli kama abiria wengine kiasi cha shilingi 2,000.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mlalamikaji akiwa amepanda ndani ya gari hilo alipewa sehemu mbele ya gari karibu na  kiti cha dreva ambaye ni mtuhumiwa wa kesi hiyo na kuulizwa na mtuhumiwa kuwa anaelekea sehemu gani ndipo mlalamikaji alimjibu kuwa anaenda Kayanga benki ya NMB na hivyo amtelemshe maeneo hayo na amlipe nauli mtuhumiwa.






Ilielezwa kuwa,  alipofika eneo hilo alidai kuwa anashida Katika maegesho ya magari Kayanga na hivyo angemtelemsha hapo na ndipo alipitiliza hadi kanisa la kathoric  la Kayanga ambapo mlalamikaji aliombwa kupewa fedha hiyo aliyo nayo kiasi cha shilingi 15.2 milioni kwa kutishiwa kupigwa risasi ndipo alipotoa kiasi hicho kwa kuhofia usalama wake na mtuhumiwa pamoja na wenzake wawili kutoroka na kutelekeza gari likiwa limepinduka kutoka umbali wa eneo la tukio.

Aidha mahakama ilieleza kwamba, mlalamikaji baada ya kunyanganywa fedha hizo alitoa taarifa kituo cha  polisi mjini Kayanga na jeshi la polisi lilimtia mbaroni mtuhumiwa akiwa amejificha kichakani katika eneo la shule ya sekondari Karagwe akiwa peke yake na akiwa ameisha badilisha nguo akijiandaa kukatiza barabara huku akiwa hana fedha hizo ambapo aligunduliwa na wachunga ng’ombe .

Hata hivyo upande wa mtuhumiwa alikana tuhuma hiyo  inayomkabili na alirudishwa rumande ambapo upande wa mahakama ulihairisha kesi hiyo kutokana na shauri hilo kuendelea kusikilizwa  mahakamani hapo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top