WAKAZI watano wa manispaa Bukoba mkoani Kagera wamefikishwa katika
mahakama ya wilaya ya Karagwe kwa tuhuma ya kosa la uchomaji wa kanisa katoriki
la kijiji cha kishoju kata ya kihanga wilayani humo na kusababisha hasara ya
shilingi milioni 52.
Mbele
ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Paul Magoryo mwendesha mashitaka wa jeshi la
polisi Inspekta Stivedana Webiro amedai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa wote
kwa pamoja walitenda kosa hilo Februali 5 mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku.
Amewataja watuhumiwa hao mahakamani hapo kwa pamoja kuwa ni Husein Omary,(33)
mkazi wa kijiji cha katoro, Abdukarim Kabaju (35) mkazi wa kata ya
Nshambya,Abdushakir Gervazi (42) mkazi wa mjini Bukoba,Yakub Swaibu(46) mkazi
wa Buyekera,na Mdashiru Wilbroad (30) mkazi wa kata ya kashai.
Washitakiwa wote kwa pamoja wamekana shitaka linalowakabili na wamerudishwa
rumande hadi juni 2 mwaka huu kesi yao itakaposikilizwa tena.
Post a Comment