Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: JUMLA YA SH 259,182,050,27 ZIMETUMIKA KUWALIPA WATUMISHI HEWA KARAGWE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Watumishi  hewa 62  wilayani Karagwe  mkoani Kagera wameigharimu  serikali  Jumla  ya  Sh 259,182 O50,27 kati  ya  hizo  zilizorejes...



Watumishi  hewa 62  wilayani Karagwe  mkoani Kagera wameigharimu  serikali  Jumla  ya  Sh 259,182 O50,27 kati  ya  hizo  zilizorejeshwa  ni Sh  30,985,441.46 ambazo  zilizokuwa zinalipwa  kwa  watumishi  hao.

Hayo  yalibainishwa  jana  na  Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  Deodatusi  Kinawiro  wakati  akisoma  taarifa  ya  wilaya  kwa  mkuu  wa  mkoa  wa  Kagera  Meja  Jenerali  Mstaafu Salum  Kijuu  katika  ziara  ya  kujitambulisha  wilayani  hapa.

Alisema  hadi  April 30,2016 wilaya  ya  Karagwe  ilikuwa  na  watumishi  hewa  62  akitoa   mchanganuo  wa  watumishi  hao  alisema   kundi la  kwanza  ni wale  ambao wapo Hospitali  Teule  ya  Nyakahanga  ni   Watumishi  hewa 36 wanaolipwa   na  serikali  kuu  kupitia  wizara  ya Afya wamebainika  ni  hewa.

Kwa  kipindi  cha  mwaka wa  fedha  2010/2011 hadi 2015/2016 fedha  zilizolipwa  ni Sh :609,785,800  baada  ya  kuondoa  makato  ya  kisheria.

Kinawiro alisema  kuwa Uongozi  wa  hospital   tayari  ulishaagizwa  kurejesha  fedha  hizo  na kuongeza  kuwa  barua  zilishapelekwa  wizara  ya  Afya ,Ofis  ya  Rais  Menejiment   ya  Utumishi wa  Umma  na Benki  ya  NMB ili  wachukue  hatua  stahiki.



Alibainisha  kuwa  kundi  la  pili  ni  Watumishi 26  wa halmashauri wa  wilaya  ya  Karagwe  waliobainika  kuwa  ni  hewa  kwa  mchanganuo  alioubainisha kuwa  watumishi 22 walibainika  kuwa  watoro  na  wameondolewa  kwenye “PAYROLL”

Watumishi 02(wawili) walibainika kuwa  walistaafu  na  waliondolewa  kwenye  “PAYROLL” fedha  zimerudishwa.

Mtumishi 01  ( mmoja) alibainika  alifariki  dunia  tarehe 10 Februari ,2016 na  alikuwa  kwenye “Payroll” ya  mwezi  machi ,2016, fedha  zilizochukuliwa  zilirudishwa

Mtumishi  mwingine 01(Mmoja) alibainika  kuwa  na  cheki  namba  mbili, fedha alizokuwa alikwisha chukua  kiasi  cha  Tshs 18,555,000  kimerudishwa  tayari.

Aidha  Mkuu  wa  wilaya ya  Karagwe  alisema  tayari  ameunda kamati  ya  watu  wanne  kuhakiki taarifa  za  watumishi  hewa ndani  ya halmashauri  ya  wilaya ,serikali  kuu  na  taasisi  zote  za serikali /umma  zilizoko wilayani  hapa.

Hata  hivyo  Mkuu  wa  mkoa  wa  Kagera  Meja  Jenerali  Mstaafu  Salum Kijuu katika  maagizo  yake  kwa  watumishi  alisisitiza suala  la  uadilifu,uwajibikaji  na  kujituma  zaidi  na  kusema  atakayeshindwa  kutimiza  hayo  hatasita  kumuondoa  mara  moja.

“Yaani  mambo  haya  ya  watumishi  hewa  yanafanyika  na  nyie  mpo  tu  sasa  mtambue  kutegea,kulindana  na  kuzembea  kwa  kipindi  hiki  hayatakuwa  na  nafasi   ni  kazi  tu”Alisema  Meja  Kijuu

Alisema   usimamizi  sehemu  za  kazi  uimarishwe  kuhakikisha  wanakomesha  tatizo  la  watumishi  hewa  na  kuongeza  muda  wa  kuwajibishana  ukifika  utawaumiza  watu  wengi ila  hamna  namna  ya  kurejesha  heshima ya  utumishi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top